Mwenyekiti wa Umoja wa dini mbalimbali Mkoa wa Singida, Hamisi Kisuke, akisoma salamu za rambirambi za umoja huo mbele ya waandishi wa habari mjini hapa kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Joseph Magufuli.
Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Alhaji Burhan Amri Mlau akisaini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Alhaj Burhan amemuelezea Dkt. Magufuli kuwa ni mtu aliyetumia uwezo wake wote wa kielimu kutafuta njia bora ya kuwatumikia watanzania na kuwainua kiuchumi.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida, Elisante John, akisaini katika kitabu hicho.
Mchungaji Rehema Gwao wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati , akisaini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Viongozi wa dini wakisubiri kusaini katika kitabu hicho.
Mwenyekiti wa Istiqaama Tawi la Singida, Khalfan Salum Khalfan, akisaini katika kitabu hicho.
Viongozi hao wa dini wakiomba dua kumuombea Rais Magufuli.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Shamim Hoza, akisaini katika kitabu hicho.
Viongozi wa dini wakisubiri kusaini katika kitabu hicho.
Mchungaji Wilson Mkoma wa Kanisa la EAGT-Puma na Katibu CPCT Mkoa wa Singida akitoa salamu za rambirambi.
Mjumbe wa Baraza la Mashehe Mkoa wa Singida, Issa Nassoro (kushoto), akizungumzia jinsi alivyo mfahamu Rais Magufuli
UMOJA wa Dini mbalimbali mkoa wa Singida, umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea majira ya saa 12:00 jjionu, tarehe 17/03/2021, katika Hospitali Nzela Dar es Salaam.
Katika salamu zetu za rambirambi tunatoa pole kwa mama Mjane Janeth J.P.Magufuli), watoto wa marehemu, ndugu jamaa na marafiki, aliyekuwa makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na watanzania wenzetu, na afrika kwa ujumla.
Tunawaomba watanzania wote hususani walioko Mkoa wa Singida, kuwa na utulivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wetu, shujaa wa Afrika. tunaamini kuwa Mungu alitupa zawadi na ni Mungu huyu huyu ameamua kumtwaa kutoka katika maisha haya sasa na mapenzi yake. tunawasihi watanzania wote kuiombea nchi ili idumu katika upendo, amani, utulivu na mshikamano huku tukisahau tofauti ztu na kusonga mbele kuyaenzi na kuyaendeleza mazuri yote aliyotuachia. pia tumuombee rehema marehemu ili afike mbinguni salama.
RAI:
Tunatoa rai kwa wote wasioitakia mema nchi yetu waliokonndani na nje ya nchi kwamba wasifikirie kuwa kuondokewa na Rais ni fursa kwao kuharibu upendo, amani, utulivu na mshikamano uliojengwa na waasisi wetu kwa muda mrefu. Mungu atuepushe na wote wenye kulitakia mabaya Taifa letu. pia tunamuombea mama yetu mpendwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kama lilivyo jina lake: Samia mwenye kusikia, atakuwa msikivu kwa Mungu na kwa wanadamu. Suluhu - kufanya suluhu/upatanisho mahali ambapo hakuna amani na Hassan maana yake kutenda mema yote aliyoyaanzisha mtangulinzi wake. mungu amvuvie Roho wake na kumvika ujasiri, akasimame kiume kwa nguvu za Mungu kuliongoza Taifa hili pasipo hofu, mashaka wala tashwishi ya aina yoyote, maana Mwenyezi Mungu atakuwa naye siku zote za uongozi wake.
No comments:
Post a Comment