TIGO PESA YAADHIMISHA MIAKA 10 YA KUFANYA MAGEUZI YA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA SIMU TANZANIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 8 March 2021

TIGO PESA YAADHIMISHA MIAKA 10 YA KUFANYA MAGEUZI YA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA SIMU TANZANIA

 

Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya Tigo pesa.Hafla hii imefanyika leo makao makuu ya Tigo Jijini Dar es salaam ,kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko Tigo, William Mpinga.


KAMPUNI inayoongoza katika kuhakikisha mtanzania anaishi maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania, leo inasherekea miaka 10 ya Tigo Pesa, huduma kamili ya kifedha inayohudumia zaidi ya wateja 9 milioni tangu kuanzishwa kwake.

Tigo Pesa imepitia mageuzi makubwa toka kuwa huduma ya kutuma na kupokea pesa hadi kuwa huduma kamili ya kifedha ikitoa huduma mbalimbali ikiwamo mikopo, bima,pamoja na malipo ya ankara.Pia, kupitia uhuishaji wa huduma (interoperability) Tigo Pesa imewezesha huduma za kutuma pesa mitandao mingine, benki, mataifa mbalimbali pamoja malipo ya Serikali (GePG) zote zikiwa za kwanza kutoka Tigo Pesa katika soko la Tanzania.



Akizungumza wakati wa hafla iliyofanyika katika makao makuu ya Tigo, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema “imekuwa safari ya aina yake ya kuboresha maisha ya mamilioni ya watumiaji wa huduma hii nchini Tanzania huku tukichangia katika agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kupitia mfumo wa ikolojia wa Tigo Pesa.”

“Huduma ya Tigo Pesa imeweza kutengeneza fursa za ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa zaidi ya mawakala 120,000 Tanzania nzima ambao wanapata kipato kupitia kuwaweesha wateja kufanya miamala mbalimbali ambapo wamepokea jumla ya Tsh 692 bilioni kama kamisheni mpaka sasa.” Alisema Pesha

“Aidha, tumewezesha mamia ya biashara kubwa na ndogo kupitia kutoa suluhu maalumu zinazowezesha kuongeza ufanisi na uzalishaji wa biashara zao na hatimaye kuchangia ukuaji wa uchumi.

Miaka kumi iliyopita, muamala wa Tigo Pesa ulimaanisha kutuma na kupokea pesa lakini leo hii Tigo Pesa imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ikitoa huduma mblimbali zinazokidhi mahitaji ya kifedha ya wateja.

Hadi mwaka huu, jumla ya Tsh110 bilioni zimetolewa kwa wateja wetu kupitia huduma ya Tigo Gawio (gawio la riba) tangu huduma hii ilipoanzishwa mwaka 2014. Hivi sasa, Tigo Pesa inafanya miamala zaidi ya bilioni moja kila mwaka ikiwa na mzunguko wa zaidi ya Trilioni 27 katika mfumo wa ikolojia wa Tigo Pesa hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi.

Kupitia azma yake ya kuleta ubunifu na kuwasikiliza wateja wetu, Tigo Pesa imefanikiwa kuleta Suluhisho mbalimbali ambazo ni za kwanza ulimwenguni ikiwamo;uhuishaji wa huduma katika soko la Tanzania na kurahisisha kufanya miamala kwenda mitandao mingine pamoja na benki,Miamala kwenda nje ya nchi,huduma ndogo za bima (Bima Mkononi) Malipo ya bidhaa kwa wafanyabiashara (Lipa Kwa Simu) pamoja na App ya Tigo Pesa.

Mbali na hayo, Tigo Pesa ni miongoni mwa kampuni zilizopewa tuzo na taasisi ya kimataifa ya GSMA, ikithibitsha usalama, uwazi na uhakika wa huduma zenye viwango vya kimataifa zinazotolewa na Tigo Pesa.

Mafanikio ya Tigo Pesa kwa muongo mmoja uliopita ni mwanzo wa kesho bora zaidi katika kuendeleza mfumo wa malipo kidigitali. Kampuni inatizamia kuifanya Tigo Pesa kituo cha huduma za kifedha kwa huduma mbalimbali ambazo zitazidi kubadilika kadiri ya muda na mahitaji ya teknolojia.” Aliongezea Pesh


Mkuu wa Kitengo cha Masoko Tigo, William Mpinga naye alisema, “Ikiwa na kauli mbiu isemayo Tigo Pesa Jana, Leo na Kesho Tunaendelea kuwa zaidi ya Pesa sherehe zitaambatana na shughuli mbalimbali na kampeni zenye lengo la kuwashukuru wadau mbalimbali wa Tigo Pesa.

 Katika kampeni ya ‘Kila mtu anashinda na Tigo Pesa’ wateja watapata bonasi hadi Sh 10,000, dakika za bure na SMS pale watakapotumia Tigo Pesa kulipa bili, bidhaa na huduma au kutuma na kupokea pesa kutoka benki au mitandao mingine ya simu.

Wateja wataingia kwenye droo ya wiki ambapo wateja 10 watapata nafasi ya 

kushinda Tsh1 milioni kila wiki na washindi 10 wa jumla watapata nafasi ya kushinda Tsh10 milioni kila mmoja katika kampeni itakayodumu kwa wiki 10 kuanzia leo.

 Pia,kutakuwa na bonasi kwa mawakala wa Tigo Pesa ambao wameweka juhudi kuhakikisha wateja wanapata huduma za uhakika kila wakati.” Alieleza Mpinga

Asante kwa kuwa nasi kwa miaka 10 ya kujifunza na kukua pamoja.Tusherekee mafanikio makubwa na tuendelee kufanya kazi pamoa kwa ubunifu zaidi ambao utarahisisha maisha ya kila siku.



No comments:

Post a Comment