NYONGO AWATAKA TBC KUONGEZA KASI KUIMARISHA USIKIVU WANACHI WAPATE HABARI SAHIHI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 12 March 2021

NYONGO AWATAKA TBC KUONGEZA KASI KUIMARISHA USIKIVU WANACHI WAPATE HABARI SAHIHI

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendelo ya Jamii Mhe. Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati hiyo kufanya ziara katika  Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Machi 12, 2021 jijini Dodoma kuona utekelezaji wa fedha zilizopatiwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa studio ya Redio Jamii jijini hapo.



Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendelo ya Jamii wakifanya ziara katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Machi 12, 2021 jijini Dodoma   kuona utekelezaji wa fedha zilizopatiwa na Serikali kwa ajili ya  ujenzi na uboreshaji wa studio ya Redio Jamii jijini hapo.

Na Shamimu Nyaki - WHUSM

                                

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendelo ya Jamii Mhe. Stanslaus Nyongo amelishauri Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutumia fedha walizotengewa kuboresha usikivu katika wilaya ambazo TBC haifiki au kuna usikivu hafifu ili wananchi wapate taarifa za ukweli na uhakika kwakua chombo hicho ndio kinachoaminika.

                                             

Mhe. Nyongo ameyasema hayo leo Machi 12, 2021 Jijini Dodoma wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwa Shirika hilo kuona utekelezaji wa ujenzi na uboreshaji wa studio ya Redio Jamii jijini hapo.

 

"TBC hongereni sana kwa ubunifu na uboreshaji mliofanya kuanzia vipindi na muonekano, hapa tumeona fedha za Serikali zimetumika ipasavyo endeleeni kutoa habari zenye ukweli kwa wananchi" alisema mhe. Nyongo.

 

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa  amesema kuwa TBC inafanya vizuri katika kuyoa habari ni chombo cha umma ambacho kinazingatia matakwa ya Katiba ya nchi ya kuhakikisha wananchi wake wanapata habari za ukweli na uhakika.

 

"Tutahakikisha maeneo yote ambayo TBC haifiki au usikivu ni hafifu tunayafikia lengo ni kuhakikisha kila mwananchi anapata habari sahihi kwa wakati" alisisitiza Mhe. Bashungwa.

 

Naye Naibu Waziri Mhe. Abdallah Ulega ameongeza kwamba TBC itaendelea kubuni na kuboresha vipindi vyake ili viwe vya kisasa na vifikie hadhira  kubwa katika kila aina ya vipindi.

 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt. Ayoub Rioba mbali na kuishukuru Kamati hiyo kwa mawazo yake, aliongeza kuwa TBC imedhamiria kuongeza Usikivu katika maeneo mengi  pamoja na kuendelea kuwekeza katika urushaji wa matangazo kwa njia ya kisasa zaidi.

 

"Tutazalisha maudhui bora na yanayovutia maana tayari tupo kidijitali, tumeanzisha Redio Jamii hapa Dodoma ambayo inapatikana katika masafa ya 93. 7  na kwasasa  itakua inapatikana mikoa ya Singida na Morogoro" alisema Dkt.Ryoba.

 

Kamati hiyo inafanya ziara ya siku mbili kuanzia leo Katika Shirika hilo kuona Utekelezaji wa fedha zilizotolewa na Serikali katika kuboresha Shirika hilo.

No comments:

Post a Comment