Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Seleman Kakoso, akizungumza na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Mhandisi Mahmoud Chamle, wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua miundombinu na vifaa vya kufundishia vya Taasisi hiyo, mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipokagua Karakana ya Reli, mkoani Morogoro.
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Mhandisi Mahmoud Chamle, akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu maboresho na ukarabati unaoendelea wa Miundombinu ya Taasisi hiyo, mkoani Morogoro.
Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Rebeka Kimambo, akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ukarabati wa majengo ya madarasa unaoendelea katika Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), mkoani Morogoro.
Amesema uwepo wa wataalam hao utaongeza ufanisi katika miradi ya ujenzi na hivyo kutekeleza kikamilifu dhana ya nchi ya viwanda kwa kuwa na wataalam wengi wa ndani katoka miradi mingi ya ujenzi.
Akizungumza mara baada ya kukagua Taasisi hiyo mkoani Morogoro, Mheshimiwa Kakoso amesema ili Taifa lifikie malengo ni vema likawekeza katika kutayarisha wataalam wengi wa kada za ufundi ili miradi mikubwa inayojengwa isimamiwe na wataalam wazalendo.
“Tuna miradi mingi ambayo inatekelezwa na Serikali na inatolewa fedha nyingi ila wanaokwenda kunufaika zaidi ni watu ambao wana level hiyo ya utaalamu wa kati na wengi wanatoka nje ya nchi, hivyo kuna umuhimu sasa wa kuwaandaa watalamu wetu wengi zaidi”, amefafanua Mwenyekiti huyo.
Aidha, ameiagiza Serikali kupitia Wizara kuongeza vifaa ambavyo vitawasaidia kuleta utaalamu sambamba na ukarabati wa miundombinu wezeshi kwa wanafunzi na wakufunzi wataopata fursa ya kupata elimu katika taasisi hiyo.
Awali akitioa taarifa ya Taasisi hiyo, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, amesema Wizara imeunganisha kilichokuwa Chuo cha Ujenzi - Morogoro (MWTI) na Chuo cha Teknolojia Stahiki ya Nguvu Kazi (ATTI) - Mbeya ili kuwa na Taasisi moja imara ya Mafunzo ya Ufundi (ICoT) itakayokuwa kituo cha umahiri katika kozi za ujenzi, umeme na mitambo na hivyo kuwezesha Taifa kuwa na wataalam wengi na mahiri wa kada za chini na za kati za ufundi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Wizara itaboresha bajeti ya taasisi hiyo ya ICoT na kuongeza wakufunzi mahiri ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati, Mkuu wa Taasisi hiyo Mhandisi Mahamoud Chamle, amesema jumla ya watumishi 109 wanahitajika ili kuiwezesha taasisi hiyo kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Katika hatua nyingine Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imekagua karakana ya kutengeneza vichwa vya treni na reli ya kisasa SGR sehemu ya Morogoro - Dar es salam na kuelezea kuridhishwa na hatua za ujenzi.
"Tumeridhishwa kwa kazi nzuri inayofanywa katika wizara hii inatia moyo", amesisitiza Mwenyekiti.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya miundombinu iko katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
No comments:
Post a Comment