Hayati, Rais John Pombe Magufuli. |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza siku 21 kuomboleza kifo cha Rais Dk. John Pombe Magufuli, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho. Katika kauli yake akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema chama kimepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa hivyo viongozi wa juu wa chama hicho walilazimika kukutana kabla ya kutoa tamko hilo.
Akimzungumzia Hayati Rais Dk. Magufuli amesema ni kiongozi wa kihistoria mzalendo wa kweli na mwenye maono atakaye kumbuka kwa mengi sana aliyolifanyia Taifa la Tanzania. Alisema JPM alikuwa mchamungu aliyejitoa kulitetea taifa na hasa kwa wanyonge. Hata hivyo amesema tayari Kamati Kuu ya Chama hicho imepanga kukutana katika kikao cha dharura jijini Dar es Salaam kwa hatua zaidi zinazofuata.
No comments:
Post a Comment