MAJALIWA AONGOZA MAPOKEZI YA MWILI WA BALOZI KIJAZI JIJINI DAR ES SALAAM - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 18 February 2021

MAJALIWA AONGOZA MAPOKEZI YA MWILI WA BALOZI KIJAZI JIJINI DAR ES SALAAM

Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi ukiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi ukiwa kwenye gari mara baada ya kupokewa kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.


WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa Februari 18, 2021 ameongoza mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Viongozi wengine walioshiriki katika Mapokezi hayo ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndubaro na Katibu Mkuu  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas.

No comments:

Post a Comment