WAZIRI AWAPA SIKU 30 WADAIWA SUGU WA TTCL, AWAONYA WAHUJUMU MKONGO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 30 December 2020

WAZIRI AWAPA SIKU 30 WADAIWA SUGU WA TTCL, AWAONYA WAHUJUMU MKONGO

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ndani ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew (kushoto).

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ndani ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba akifuatilia.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile (kushoto) kuhusu mitambo ya zamani ya Shirika hilo katika ziara ya waziri kutembelea TTCL.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) kuhusu mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wakati wa ziara yake kwenye Shirika hilo, Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo A. Mathew akifuatilia.



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya ziara ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) alipotembelea shirika hilo.



Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile pamoja na Naibu Waziri na Menejimenti ya Wizara hiyo katika mkutano na waandishi wa habari.

Na Joachim Mushi, Dar 

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile ametoa mwezi mmoja kwa taasisi zote za umma, binafsi na watu wengine wote wadao daiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuhakikisha wanalipa mara moja madeni yao, la sivyo TTCL itasitisha huduma kwa wateja hao.

Waziri Dk. Ndugulile ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara yake ndani ya TTCL akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew pamoja na menejimenti ya wizara ambapo alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa TTCL, Wafanyakazi na Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi hiyo. 

"Nimepokea taarifa kuwa kuna madai na madeni mengi sana, wanazidai taasisi mbalimbali za umma na za binafasi, Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambao ndio uti wa mgongo wa mawasiliano ya nchi yetu ni kitu ambacho serikali limegharamia fedha nyingi kuujenga na hata sasa kuuhudumia kwa hiyo taasisi zote zinazopata mawasiliano ya intaneti na huduma nyingine toka katika mfumo huu wa mawasiliano zinawajibika kulipia gharama na tozo wanazopatiwa na TTCL," alisema Waziri Dk. Ndugulile.

"...Ifikapo tarehe 31 ya mwezi Januari 2021 wadaiwa wetu sugu wote wawe wamelipa hizo fedha na wale ambao watakuwa hawajalipa basi wakatiwe mawasiliano hayo ya mtandao ili mpaka pale watakapoweza kuzilipa hizo fedha. Natumia nafasi hii kuzihimiza taasisi zote za umma kwamba ifikapo tarehe 31, Januari 2021 ziwe zimekamilisha malipo hayo ya zaidi ya bilioni 30 ambazo tunadai kwa taasisi mbalimbali."

Alisema zipo taasisi ambazo zinafanya makusanyo makubwa sana kwa siku; ..mtu anakusanya milioni 100 lakini anashindwa kulipa milioni 2 za huduma ambazo sisi tunampa na ndizo zinazomsaidia yeye kukusanya mapato, hii ni kutotutendea haki, hivyo sisi kama wizara tumeona tunawajibika kama wizara nyingine zinazotoa huduma kwa taasisi nyingine," 

Pamoja na hayo ameielekeza wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kufanya (NBS) kwa pamoja kufanya tathmini ya kina ili kupata uhalisia wa mchango wa tehama ndani ya nchi na kujua ni kiasi gani. Hii ni pamoja na kujua ni kiasi gani kinapatikana moja kwa moja katika mapato ya simu, kiasi gani pia mifumo ya tehama inachangia katika mapato ndani ya Serikali.

"...mfano sasa hivi tunajua mapato ya Serikali kupitia GPG na sisi tuna mchango wetu kule, kuna taasisi ambazo zinafanya makusanyo ya siku kama bandarini, Polisi nasisi tuna mchango wetu kule. "...Alisema zoezi hili lina lengo la kujua mchango wa sekta ya tehama kiuhalisia mchango wa tehama ndani ya taifa letu ni kiasi gani, kiasi gani kinatokana na mapato ya moja kwa moja kama matumizi ya simu na kiasi gani kinatokana.

Aidha akizungumzia kundi la watu wanaohusika na kuhujumu miundombinu ya mawasiliano, ukiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; amesema wamepanga kufanya msako mkali kuwabaini wauzaji, wanunuzi na wote wanaohusika ili kuwachukulia hatua kali za kisheria. Aliongeza kuwa kundi hili litausisha pia washindani wa biashara wa TTCL ambao wamekuwa wakihujumu miundombinu ili kulidhohofisha shirika hilo.

"...Tumebaini kuwa kuna hujuma ambazo zinafanyika katika miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, baadhi ya watu kuiba na kukata nyaya za Mkongo na kwenda kuziyeyusha kupata madini ya kopa, naomba niwakumbushe hivi karibuni Serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ilifanya msako mkali kwa watu wote ambao wanauza vyuma chakavu vinavyotokana na reli ili kubaini wanao hujumu miundombinu. 

Tutafanya hivyo nasisi kutafuta mtu yeyote mwenye nadini yanayotokana na miundombinu yetu na kuchukua hatua kali za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi, mkongo huu tumeujenga kwa gharama kubwa sana hatuwezi kukubali watu wachache wenye nia ovu kuendelea kulihujumu taifa," alisema Waziri.

No comments:

Post a Comment