TRAA YAIPONGEZA SERIKALI KUIBUA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA NJE NA NDANI YA NCHI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 28 January 2026

TRAA YAIPONGEZA SERIKALI KUIBUA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA NJE NA NDANI YA NCHI


Mwenyekiti wa TRAA, Abdallah Mohamed akizungumza siku ya kuwaaga vijana 109 kwenda kufanya kazi Saud Arabia.

NA DUNSTAN MHILU

MWENYEKITI wa Asasi za Ajira Tanzania (TRAA) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya usafirishaji ya AL-Mahal Travel, Abdallah Mohamed Khald amesema serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa awamu ya Sita wa Dk, Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ya kuibua fursa za ajira kwa vijana nchini na nje ya nchi.

Mkurugenzi huyo aliyasema hayo alipozungumza ofisini kwake jijini Dar es salaam kuhusu mwenendo wa ajira nchini kwakuwwa yeye ,kampuni yake na Traa anayoisimamia ni muumini na mdau mkubwa wa maendeleo na unapozungumzia maendeleo huwezi kuzungumzia ajira.

“Nikili kwamba seriakali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa sana katika uibuaji wa ajira serikalini na katika sekta binafsi,nayasema haya kwa sababu muhimu na nyeti, wakati wa utawala wa Hayati Dk Magufuli kulikuwa na ushirikishwaji mdogo kwa sekta binafsi lakini Mama ameuboresha’’ alisema Khald

“Nachelea kusema hivyo siyo kwa nia mbaya na nnaomba nsinukuliwe vibaya, mathalani katika sekta ya usafirishaji ambayo ninahudumu hususani katika kuwatafutia vijana nje ya nchi, kutokana na mapungufu mengi yaliyoonekana hapo nyuma Dk Magufuli alipiga marufuku kusafirisha vijana wa kitanzania kwenda ughaibuni kufanya kazi zilizoitwa zisizo na staha hadi changamoto zote zishughulikiwe” alisema Khald

Katika chagizo hilo Khald alisema kwamba baada ya Rais Samia kuingia madarakani mawakala wenye nia njema na vijana wakitanzania na serikali yao waliamua kufanya mazungumzo na serikali na hivyo kuamriwa kwamba mawakala wasifanye kazi kiholela balia washirikiane na serikali kupitia wizara ya ajira,vijana na mahusiano ambayo ni wizra mpya kuwahi kuundwa nchini.

Aidha Khald alisema kutokana jitihada hizo milango ya fursa za ajira nje ya nchi zimefunguliwa na Kampuni ya Al-Mahal Traveler imekwisha saini zaidi ya mikataba sita nchini Dubai kwa ajili ya uaminifu wake kimataifa.

Sanjali na hilo TRAA pia imesafirisha vijana 109 kwenda nchini Dubai mwezi Januari mwaka huu kufanya kazi mbalimbali  ambapo Rais aliahidi ndani ya siku miamoja atatangaza ajira serikalini na sekta binafsi ambapo serikali yake na sekta binafsi zitashirikiana kutafuta fursa za ajira ndani na nje ya nchi.

“Hili ni bayana  tayari tuna kundi la vijana madereva 500 wataondoka hivi karibuni kwenda nchini Dubai kwa ajili yakufanya kazi katika makampuni mbalimbali na tunatambulika kimataifa kama Kampuni chini TRAA pia kama watoa huduma stahiki na zenye staha,kwakweli mama apewe maua yake ,Rai kwa vijana wasisite kutembelea ofisi zetu zetu zilizopo jengo la Salamanda Dar es Salaa barabara ya Samora na Mkwepu.

No comments:

Post a Comment