TIGO IMEZINDUA KAMPENI YA KUFUNGA MWAKA KWA STAILI YAKE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 8 December 2020

TIGO IMEZINDUA KAMPENI YA KUFUNGA MWAKA KWA STAILI YAKE

Meneja Vifaa vya Intaneti wa Tigo, Mkumbo Myongan akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya kwa ajili ya kuhakikisha wateja wake wanafurahia kipindi cha mwisho wa mwaka.Uzinduzi huu umefanyika mapema leo Jijini Dar es salaam.

Meneja Uhusiano kutoka TECNO, Eric Mkomoye akifafnua jambo kwa waandishi wa habari mapema leo mara baada ya zinduzi wa kampeni mpya kwa ajili ya kuhakikisha wateja wake wanafurahia kipindi cha mwisho wa mwaka.Uzinduzi huu umefanyika mapema leo Jijini Dar es salaam.


•Wateja watapata fursa ya kujishindia pikipiki au TV ya kisasa.

KAMPUNI inayoongoza katika kuhakikisha mtanzania anaishi maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania, leo imezindua kampeni mpya kwa ajili ya kuhakikisha wateja wake wanafurahia kipindi cha mwisho wa mwaka.

Kampeni hii imezinduliwa baada ya awali kuzindua kampeni nyingine ya Jaza Tukujaze Tena.

Katika kipindi cha wiki sita cha promosheni hii, wateja wa Tigo watakaonunua  simu janja za ITEL T20 au Tecno Kitochi 4G Smart watapata data ya  GB30 kwa mwaka mzima na wakati huo huo wataingia kwenye droo ya  kujishindia kati ya pikipiki au Smart TV.

Meneja Vifaa vya Intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, alisema kuwa promosheni hiyo ni mwendelezo wa kuufanya mwisho wa mwaka 2020, kukumbukwa na wateja wa Tigo.

“Tigo kama mtandao unaoongoza katika mageuzi ya kidijitali, umekuwa ukivutia wateja wake kila wakati. Kutokana na hilo, tumeamua kuja na promosheni hii ya simu janja ili kurahisisha zaidi maisha ya wateja wetu katika kipindi hiki,”.

"Tuna imani kubwa kwamba promosheni hii itawasaidia wateja wengi wa Tigo kufurahia manufaa ya ITEL T20 na  Tecno Kitochi 4G Smart zinazopatikana kwa sh. 84,900 na 45,000, ikijumuishwa na data ya bure ya hadi GB 30 kwa mwaka mzima," alisema.Myonga.

"Ni utamaduni wetu pia kutoa ofa za simu janja kwa wateja wetu katika kipindi cha msimu wa mwisho wa mwaka.

" Hivyo ninawaomba wateja wetu wote ikiwemo wale wanaosafiri kwenda ndani na nje ya nchi, wanaoenda kuungana na familia zao katika kipindi cha mwisho wa mwaka, kuchangamkia fursa kwani wanaweza kushinda kati ya pikipiki na Tv ya kisasa na kwenda kutoa zawadi kwa familia zao,". aliongeza Myonga.

Meneja Uhusiano kutoka TECNO, Eric Mkomoye alisema, “Azimio letu ni kufanya maisha ya mteja kuwa ya kidigitali zaidi, kama chapa inayojighushisha na Simu janja, tungependa watanzania wote waishi maisha ya kidigitali, na ndio sababu tumeshirikiana na Tigo kwaajili ya kuwaletea simu za bei nafuu kama Kitochi na T20 simu zote mbili zikiwa zina uwezo wa teknolojia ya 4G, kwaajili ya wateja kufurahia kuzitumia katika msimu huu wa siku kuu.”

Tunaomba wateja wote wa Tigo kuendelea kujiunga na kutumia simu janja kwa ajili ya kurahisisha maisha.

 

No comments:

Post a Comment