Afisa kutoka Benki ya NMB,Salma Chiwanga ametumia nafasi hiyo kufafanua kwa kina namna ambavyo benki hiyo imekuwa karibu na wanawake hasa katika kuwawezesha kutimiza ndoto zao kupitia shughuli wanazozifanya.
"Benki yetu ya NMB imeamua kuwasaidia wajasiriamali wanawake , tunacho kifurushi maalum ambacho kinamlenga wanawake wafanyabiashara wadogo na wale wafanyabiashara endelevu, kwetu sisi NMB kuna mwanamke jasiri na hivyo kuna kifurushi kinachomtosheleza mwanamke jasiri.
"Kifurushi hicho kina huduma za NMB mkononi , huduma za pamoja akaunti, tuna huduma za fanikiwa akaunti na dunduliza.Wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo hasa wanawake tunawaambia watumie benki ya NMB kwasababu mpaka sasa benki hiyo imewapa kipaumbele kikubwa sana wafanyabiashara wadogo wadogo na wajasiriamali.
"Ahadi yetu kwa wateja wao ni kwamba mteja wao yoyote atakapokuwa amejiunga na huduma zetu na hasa atapofungua akaunti ataunganisha kwenye klabu ya wanawake ya Amka Twende Women,"amesema.
Mkazi wa Kimara Jijini Dar es salaam ,Vailet Maira akifungua Chap Chap Instant Account alipotembelea kwenye banda la NMB katika hafla ya
kukabidhiwa fedha kwa Shule ya Msingi Sinza Maalum ambazo zinakwenda kufanikisha ujenzi wa vyoo na bafu kwenye shule hiyo hafla hiyo ilifanyika Katika viwanja vya Non Bosco jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi wa hafla ya kukabidhiwa fedha kwa Shule ya Msingi Sinza Maalum,Diwani wa Kata ya Kijitonyama Dama Lusangija(kushoto)akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Benk ya NMB,Salma Chiwanga namna ya kufungua CHAP CHAP Akaunti ambayo bora na nafuu inayomuwezesha mteja kufanya shughuli zake zote za kibenki papo kwa papo bill shida popote alipo kwa kutumia Simu ya mkononi kupitia Huduma ya NMB Mobile.
hafla hiyo ilifanyika Katika viwanja vya Non Bosco jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment