Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye uzinduzi huo. |
BENKI ya NMB imezindua klabu maalumu ya wanawake waliyoipa jina la Mwanamke Jasiri, yenye lengo la kuwahimiza wanawake kutambua fursa mbalimbali zilizopo ndani ya NMB kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City- Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Huduma Jumuishi wa NMB – Nenyuata Mejooli alisema kuwa, NMB kwa kutambua na kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya Taifa letu, imezindua klabu hiyo ikiwa ni mkusanyiko wa bidhaa na huduma mbalimbali zinazoweza kuwasaidia wanamke kiuchumi na kuwainua kibiashara na kuwaonyesha fursa wanazoweza kuzipata kupitia NMB.
Kwa kifupi tu, bidhaa ambazo zipo katika kifurushi cha jasiri ni Fanikiwa Akaunti, Pamoja Akaunti, Mikopo ya wanawake waajiriwa (SWL), NMB Mkononi, Bima, Dunduliza na kadhalika.
Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Jaji wa Mahakama wa Rufani Tanzania Mhe. Jaji Joaquine De Mello aliipongeza Benki ya NMB kwa kuaamini kuwa wanawake nchini wakiwa kitu kimoja, wakajua fursa zilizomo ndani ya benki ya NMB kama vile mikopo na elimu ya biashara; wanaweza kutumia kwa maendeleo binafsi, familia zao na taifa kwa ujumla, ambapo watakua wametoa mchango mkubwa na mwisho kulikomboa taifa hili kiuchumi.
Hafla hiyo, iliwakunaisha Wakinamama Wajasiriamali na Wafanyabiashara zaidi ya 170 akiwemo Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NMB - Mama Margaret Ikongo, walioshiriki katika mdahalo wenye mada zilizokuwa chachu ya mambo muhimu juu ya ushiriki wa mwanamke katika huduma rasmi za kifedha ili kuhakikisha mwanamke anapata huduma za kifedha kwa urahisi na kwa usalama.
Pia walitumia fursa hiyo kufahamiana, kubadilishana mawazo na zaidi kuonana na watalaam wa Benki ya NMB kufahamu zaidi kuhusu huduma na bidhaa mbalimbali za NMB. Ahadi ya NMB ni moja tu, kutoa huduma nzuri za kibenki, zenye tija na zinazoendana na mahitaji ya wanawake nchini.
No comments:
Post a Comment