TANZANIA PRISON YAWAPA FURAHA MASHABIKI NDANI YA NELSON MANDELA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 23 October 2020

TANZANIA PRISON YAWAPA FURAHA MASHABIKI NDANI YA NELSON MANDELA

Beki wa Timu ya Tanzania Prison  Michael Ismail akisalimia washabiki wa timu hiyo waliofika kushuhudia ushindi wa Tanzania Prison dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC.

Beki wa Timu ya Tanzania Prison  Michael Ismail akisalimia washabiki wa timu hiyo waliofika kushuhudia ushindi wa Tanzania Prison dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC.

HATIMAYE timu ya Tanzania prison imekata kiu ya mashabiki wao waliokuwa na hamu ya kuifunga timu ya Simba na hatimae kujiweka mahala pazuri katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara katika mzunguko wa sita hali ilimpelekea mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo kutoa neno kwa wanarukwa.

Mh. Wangabo alisema kuwa amefurahi kwa timu hiyo  ya Tanzania Prison kuufanya uwanja wa Nelson Mandela na timu hiyo ilisema kuwa ina deni kubwa kwa wanarukwa na hatimae imefanya juhudi ya kupata ushindi mwanana na kila mtu amefurahi.


“Furaha ya mchezo ni kushinda na ili uweze kupata mashabiki wengi ni lazima ushinde na kama ushindi wanakuja kufanya nini kiwanjani, kwahiyo huu ni mwanzo sasa uwanja utakuwa unafurika kama ulivyoona leo uwanja ulikuwa haujatapika vizuri kwasababu mechi zimegonganishwa, Yanga inacheza huku na Simba inacheza huku, watazamaji ikawa kama ulivyoona,” Alisema.


Kwa upande wake kocha msaidizi wa Tanzania Prison Shaaban Kazumba alisema kuwa tangu awali walikuwa wamewasoma simba hasa baada ya kuwafunga timu ya jeshi wenzao na hivyo kuwafanya wawe makini Zaidi wakati wakijiandaa na mechi hii ya leo.


“Unapocheza na timu ni lazima uwe na Discipline kwasababu kwanza unacheza na bingwa na unajua kuwa unacheza na timu yenye wachezaji mahiri na tumeshakutana nao siku nyingi, wamewafunga wenzetu  wa jeshi JKT goli tatu katika uwanja wa Dodoma na hivyo tulichukua ile video na kuwasoma,” Alisisitiza.


Halikadhalika kocha wa Simba SC Sven Vandebroek alikubali kipigo hicho ndani ya Sumbawanga na kuahidi kujipanga katika mechi nyingine zijazo.


Goli la Tanzania Prison lilifungwa katika kipindi cha pili dakika ya 48 na mfungaji akiwa Samson Mbangula, goli lililowainua washabiki wa Tanzania Prison na kushindwa kukaa chini hadi mwisho wa mchezo Tanzania Prison 1 na Simba SC bila ya goli.

No comments:

Post a Comment