Mgombea
udiwani wa Kata ya Mzizima Fredrick Chiluba kushoto akimuombea kura
mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia wakati wa
mkutano wake wa kampeni. |
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na mgombea
udiwani wa kata ya Mzizima Fredrick Chiluba wakifuatilia matukio
mbalimbali kwenye mkutano huo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba. |
Msanii Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo. |
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema akichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha anajitahidi kuanzisha ujenzi wa hosteli kwa wanafunzi wanaosoma shule za sekondari wanaokaa mbali ili kuwawezesha kusoma bila uwepo wa vikwazo.
Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule za Sekondari kukaa mbali na maeneo ya shule hali inayopelekea kushindwa kufika kwa wakati kutokana na changamoto ya usafiri.
Ummy aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mzizima katika uwanja wa Gogovivu kwenye mkutano wake wa kampeni ambapo alisema suala hilo litakuwa mwarobaini wa kuwaepusha wanafunzi kutokufika shuleni.
“Ninaamini
ujenzi wa Hostel utasaidia kupunguza changamoto ambazo zinawakabili wanafunzi
wanaosoma shule za mbali kutokana na kukosekana kwa usafiri kwa baadhi ya
maeneo wanayokwenda”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba ataendelea pia kushirikiana nao kujenga miundombinu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.
“Ninafahamu shule za msingi Mafuriko,amboni,rubawa na mleni kuna maadhibi miomdnboni sio mizuri na madarasa hayatoshi,ninawaomba sana ..mchango wangu niliiutoa kabla sijawa mbunge niaminini niweze kushirikiana nanyi kuboresha elimu hasa miundombinu na kutafuta madawati kwa ajili ya wanafunzi”Alisema Ummy
“Lakini pia sijaisahau shule ya sekondari Kiomoni nimewekeza ujenzi wa madarasa mawili ninawaomba sana mnichague ili tuweze kuiboresha zaidi”Alisema
Hata hivyo alisema pia atalazimika kubadilisha jina la shule ya sekondari Kiomoni kwa sababu ni ya shule ya kata ya Mzizima hivyo watabadilisha jina liweze kuwa shule ya sekondari Mzizima.
“Niaminini tuweze kutatua changamoto za wanafunzi wa Rubawa,Mleni ambao wanakwenda mpaka sekondari ya kiomoni kwa usafiri wenye changamoto na kupelekea kushindwa kufika shuleni kwa wakati,”Alisema.
No comments:
Post a Comment