WAZIRI DKT. SIRA AFUNGUA MAONESHO YA SIKU YA USAFIRI KWA NJIA YA MAJI YANAYOFANYIKA KITAIFA, WILAYANI KYELA, MKOANI MBEYA. - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 24 September 2020

WAZIRI DKT. SIRA AFUNGUA MAONESHO YA SIKU YA USAFIRI KWA NJIA YA MAJI YANAYOFANYIKA KITAIFA, WILAYANI KYELA, MKOANI MBEYA.

 

Wananchi mbalimbali wa Kyela Mkoani Mbeya, wakiangalia ndege isiyo na rubani (Drone) ya Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) katika maonesho ya siku ya usafiri kwa njia ya maji yanayofanyika kitaifa, Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.


Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe Dkt. Sira Ubwa (aliyevaa hijabu) akimsikiliza Baharia kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kamandi ya Wanamaji, Idara ya Uokoaji (NAVY), Mwanaisha Abdallah (kushoto), kuhusu matumizi ya vifaa vya kujiokoa, wakati Waziri huyo alipotembelea banda la Jeshi hilo, katika maonesho ya siku ya usafiri kwa njia ya maji yanayofanyika kitaifa, Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.


Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe Dkt. Sira Ubwa (wa pili kulia) akimsikiliza Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) Hussein Makame  kuhusu matumizi ya ndege zisizo na rubani katika ulinzi, wakati Waziri huyo alipotembelea banda la Kikosi hicho, katika maonesho ya siku ya usafiri kwa njia ya maji yanayofanyika kitaifa, Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kita.


Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe Dkt. Sira Ubwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira-Uchukuzi, Bi Stella Katondo, akifafanua kuhusu siku ya usafiri kwa njia ya maji, alipotembelea banda la sekta hiyo katika maonesho ya siku ya usafiri kwa njia ya maji yanayofanyika kitaifa, Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.


Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe Dkt. Sira Ubwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mabaharia Nchini (TASU) Kapteni Josiah Mwakibuja, baada ya kuwasili kwenye ufunguzi wa maonesho ya siku ya usafiri kwa njia ya maji yanayofanyika kitaifa, Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment