UCHAGUZI UKIFANYIKA LEO JPM ANASHINDA KWA ASILIMIA 88 - POLEPOLE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 11 September 2020

UCHAGUZI UKIFANYIKA LEO JPM ANASHINDA KWA ASILIMIA 88 - POLEPOLE

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg Humphrey Polepole akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mjini Chato, mkoa wa Geita, Ijumaa Septemba 11, 2020.
                                      

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg Humphrey Polepole akiongea na wanahabari mjini Chato, mkoa wa Geita, Ijumaa Septemba 11, 2020.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg Humphrey Polepole akiongea na wanahabari mjini Chato, mkoa wa Geita, Ijumaa Septemba 11, 2020.

Na Joachim Mushi

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Humphrey Polepole amesema kwa namna ambavyo mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli anavyokubalika na wananchi tangu wameanza kampeni zao, wananchi wakipiga kura leo anaibuka mshindi kwa asilimi 88.

Ndg. Polepole ameyasema hayo leo mjini Chato, mkoani Geita alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni mapumziko yao mafupi kabla yakuendelea na kampeni baada ya kufanya kampeni kwa siku 10 mfululizo mikoa kadhaa wakinadi ilani ya CCM kwa wananchi maeneo hayo.

"...Yaani ikitokea kura zikapigwa leo hii, mgombea wetu ambaye pia ni Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anaibuka na ushindi kwa asilimia zaidi ya 88. Hii ni kutokana na mambo makubwa ya kihistoria ambayo amelifanyia taifa hili na namna alivyopokewa na kuungwa mkono na wananchi katika kampeni zake tangu tumeanza...," alisema Ndg. Polepole akizungumza na wanahabari.

Amesema mgombea wa CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli amefanya mambo mengi katika sekta mbalimbali tangu aingie madarakani jambo ambalo limeiwezesha nchi sasa kuingia katika orodha ya nchi ya kipato cha kati.

Alisema Serikali ya awamu ya tano mbali na kutoa elimu bure na kuboresha huduma za afya mara dufu kuanzia madawa, vifaa tiba, ujenzi wa zahanati, hospitali na vituo vya afya kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa, kikanda na taifa kwa ujumla mpango wa sasa kuleta huduma za bima kwa wananchi wote.

Aliwashangaa wanaopinga ujenzi wa viwanja vya kisasa vya ndege mikoa mbalimbali unaofanywa na Serikali ya JPM na kudai watu hao hawana nia njema na taifa. Aliongeza kuwa Serikali imenunua ndege ambazo zinapaswa kutoa huduma kwa Watanzania wote sasa ujenzi wa viwanja vipya vya kisasa vya ndege na ukarabati utawezesha ndege hizo kutoa huduma kila mkoa tofauti na hapo awali.

Amesema Serikali ya CCM tangu JPM aingie madarakani imejenga viwanja vye ndege vya kisasa takribani 11 mikoa mbalimbali na kukarabati baadhi, ikiwemo mikoa ya Tabora, Mtwara, Kigoma, Shinyanga na pamoja na Bukoba. Aidha alitolea mfano kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa mkoani Mwanza umeufungua mkoa huo kibiashara za kimataifa jambo ambalo limeleta mabadiliko makubwa kiuchumi.

"...Kwa mambo makubwa aliyoyafanya mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli yanamfanya Mtanzania mpenda maendeleo na mzalendo anayelitakia taifa letu maendeleo kumpigia kura ya ndio ili aendelee kufanya makubwa zaidi," alisema Polepole.

Umati wa wananchi wakimpokea mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli njiani kabla ya kufanya mkutano wake wa kampeni.

Maelfu ya wananchi wakimsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni mikoani.

Maelfu ya wananchi wakimsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni mikoani.


No comments:

Post a Comment