DC CHEMBA, TENMET WAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI CHANGAMOTO ZA ELIMU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 19 August 2020

DC CHEMBA, TENMET WAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI CHANGAMOTO ZA ELIMU

Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Chacha (kushoto) akihamasisha wananchi katika ushiriki wa utatuzi wa changamoto mbalimbali za elimu kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu yalioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) yakifanyika Tarafa ya Kwamtoro, Shule ya Sekondari Kwamtoro.


Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga akizungumza na jamii waliposhiriki shughuli za ujenzi wa bweni la wanafunzi katika eneo la Shule ya Sekondari Kwamtoro, ambapo kwa pamoja walishiriki na wananchi kuchimba mashimo ya vyoo, kubeba mawe na mchanga kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Chacha (kulia) akihamasisha wananchi katika ushiriki wa ujenzi wa bweni la wanafunzi katika eneo la Shule ya Sekondari Kwamtoro, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu yalioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET).


Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Chacha (katikati) akimkabidhi zawadi mmoja wa wazazi wa mfano katika ushiriki wa wazazi kwenye shughuli za maendeleo ya elimu Shule ya Sekondari Kwamtoro.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi wa Juma la Elimu Tanzania, Anna Sawaki akizungumza na wanafunzi eneo la Shule za Msingi na Sekondari za Kwamtoro.


Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakiwasili eneo la ujenzi wa Bweni la wanafunzi kushiriki ujenzi wa kujitolea.


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwamtoro, Neema Muna (wa pili kushoto) akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa Bweni la Wanafunzi, shuleni hapo. 


Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga (kulia) akizungumza jambo alipokagua hatua za ujenzi wa Bweni la Wanafunzi Kwamtoro kabla ya kushiriki katika ujenzi na kuchangia fedha katika ujenzi huo.


Baadhi ya wananchi wa Kwamtoro wakishiriki katika ujenzi wa vyoo vya Bweni la Wanafunzi, Sekondari ya Kwamtoro.


Sehemu ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakishiriki shughuli za ujenzi wa Bweni la Wanafunzi Sekondari ya Kwamtoro.


Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga (kulia) akiwaongoza wananchi walojitokeza kushiriki shughuli za ujenzi wa Bweni la Wanafunzi Sekondari ya Kwamtoro.


Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Chacha (kulia) akihamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii ili wafikie malengo yao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu yalioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET).


Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Chacha (kushoto) akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kwamtoro aliyefanya vizuri katika masomo yake.


Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga akizungumza na jamii mara baada ya kushiriki shughuli za ujenzi wa bweni la wanafunzi katika eneo la Shule ya Sekondari Kwamtoro.

Na Joachim Mushi, Chemba

MKUU wa Wilaya ya Chemba, Simon Chacha kwa kushirikiana na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wamehamasisha wananchi Tarafa ya Kwamtoro kushiriki katika kutatua changamoto za elimu katika maeneo yao ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali.

Tukio hilo limefanyika kwa vitendo katika eneo la Shule ya Sekondari Kwamtoro, ambapo kwa pamoja walishiriki na wananchi kuchimba mashimo ya vyoo, kubeba mawe na mchanga kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi la Sekondari hiyo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo ambayo ni mwendelezo wa maadhimisho ya  Juma la Elimu mwaka huu, wilayani Chemba, Bw. Chacha aliwataka wazazi n jamii kushiriki katika utatuzi wa changamoto za elimu kwenye maeneo yao. Alisema Serikali kwa nafasi yake inajitahidi kutatua changamoto za elimu kila zinapojitokeza, lakini wananchi ambao familia zao ni wanufaika moja kwa moja wanakila sababu ya kushiriki ana na Serikali.

"...Mfano mzuri tunauona hapa Kijijini kwenu Serikali imeleta fedha za awali kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi Sekondari ya Kwa mtoro ujenzi huu umesuasua kwasababu ya ugumu wa wazazi na jamii kujitolea kupunguza gharama, jambo hili ni kuikatisha serikali tamaa, naombeni sasa tubadilike tushirikiane maana wanufaika wa kwanza ni familia zetu," alisema Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Bw. Chacha akizungumza katika hafla hiyo.

Kwa upande wake, Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga ambao walishiriki shughuli za ujenzi wa bweni hilo, alisema wameamua kuja kuhamasisha jamii kushiriki katika utatuzi wa changamoto za elimu ili kuleta mabadiliko ya kimtazamo hasa maeneo ambayo hayafanyi vizuri kiufaulu ikiwemo Chemba.

Alisema mbali na wanachama wa TENMET kushiriki kwa vitendo kwenye ujenzi huo, wamechangia pia fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni nane pamoja na kutoa mifuko 2oo ya simenti isaidie ujenzi kwa bweni hilo na maeneo mengine yanayoitaji msaada huo. 

Katika kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu masuala ya elimu TENMET ilitoa zawadi za vitabu na madaftari kwa wanafunzi waliofanya vizuri kimasomo katika shule ya Msingi na Sekondari Kwamtoro, na pia kutoa zawadi kwa wazazi wa mfano walioonekana kushiriki vizuri.


No comments:

Post a Comment