BANDA LA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO LIMEKUWA KIVUTIO MAONESHO YA NANENANE KITAIFA SIMIYU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 3 August 2020

BANDA LA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO LIMEKUWA KIVUTIO MAONESHO YA NANENANE KITAIFA SIMIYU

Mtaalamu wa Huduma Ndogo za Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Janeth Hiza (kushoto), akitoa elimu ya Sheria ya huduma hiyo kwa wanawake kutoka Bariadi Mkoani Simiyu walio katika vikundi mbalimbali vya VICOBA, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Wakazi wa Mkoa wa Simiyu Bi. Mwinza Maghembe na Mbula Mayenga, wakipewa elimu ya huduma ndogo za fedha kutoka kwa Mtaalamu wa Sekta hiyo wa Wizara ya Fedha na Mipango. Bi. Limi Burugu (kushoto), walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Wakazi wa Bariadi Mkoa wa Simiyu (kushoto) wakipewa maelezo juu ya mifumo ya malipo ya Serikali kutoka kwa mtaalamu wa mifumo hiyo wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Chilumba, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Mtaalamu wa Sheria kutoka Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), Bw. Amosi Manyama (kulia), akitoa maelezo kuhusu utaratibu wa kujiunga na Chuo hicho na Kozi zinazopatikana kwa wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Bw. Peter Mayila, akisikiliza kwa makini maswali ya Bw.  Benedicto Wilison, kuhusu majukumu ya Wakala huo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

No comments:

Post a Comment