![]() |
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria katika shughuli za kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
|
![]() |
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria katika shughuli za kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
|
![]() |
Familia ya Hayati Mkapa pamoja na Rais Dk. Magufuli wakielekea kutoa heshima za mwisho. |
![]() |
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete pamoja na familia yake wakitoa heshima ya mwisho. |
![]() |
Sehemu ya uwanja kwa juu kama inavyoonekana ambapo shughuli za kuagwa sinafanyika. |
Na Joachim Mushi, Dar
RAIS Dk. Magufuli amesema Hayati Mkapa atakumbukwa kwa mengi, ikiwemo kuwa na uongozi bora ulioiletea nchi maendeleo, kuwa baba wa demokrasia kwa kuiboresha, ameweza kudumisha amani ndani na nje ya Tanzania, msuluhishaji wa migogoro mingi kimataifa na muibuaji mzuri wa viongozi wa taifa.
Rais Magufuli amesema Hayati Mkapa ni baba wa demokrasia kwa kuwa ndiye rais wa kwanza nchini kuingiza taifa katika uchaguzi wa vyama vingi bila machafuko na ameonesha msuluhishi wa migogoro ya nje kwa mafanikio kwani amesuluhisha nchi za Rwanda, Kenya, Burundi na Demokrasia ya Congo hivyo mchango wake umeacha alama nje na ndani ya taifa.
Amesema kiongozi huyo ameanzisha taasisi nyingi za umma akiwa madarakani ikiwa ni jitihada za kusaka maendeleo ya nchi na uboreshaji utawala bora nchini, kama vile kuanzisha TAKUKURU, kuanzisha TRA, Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Mamlaka ya Mafuta (EWURA), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya SUMATRA na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Mamlaka za Maji Safi na Taka pamoja na Wakala wa Barabara (TANROADS)
Aidha amesema mchango alioutoa hayati Mkapa kwa Tanzania hauwezi kusahaulika, hivyo Serikali yake itafanya kila jitihada kuhakikisha inadumisha na kuyaenzi mazuri yote yaliofanywa na kiongozi huyo mstaafu wa taifa la Tanzania. Alisema Hayati Mkapa ni muibuaji mzuri wa vipaji vya uongozi na hasa viongozi wa taifa, kwani ndiye aliyemuibua Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, alimuibua Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na wengine wengi.
Rais Magufuli pia amebainisha hata yeye ameibuliwa na Hayati Mkapa, kwani bila yeye asingelionekana na hata kufikia ngazi aliyonayo kwa sasa (Rais wa nchi). Mkapa ni shujaa wangu...ni mtu muhimu sana katika maisha yangu, hata nilipopata shida hakuniacha hakutaka nianguke hivyo kuondoka kwake ni pigo kubwa kwangu," alisema Rais Magufuli huku akifuta machozi mara kadhaa kwenye hotuba yake kumwelezea Hayati Mkapa.
Rais Dk. Magufuli alitangaza rasmi kuwa uwanja wa taifa wa michezo wa jijini Dar es Salaam kuanzia sasa uitwe Uwanja wa Mkapa ili kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo. Mwili wa Hayati Mkapa umesafirishwa leo kuelekea Kijijini alipozaliwa Lupaso, Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kwa ajili ya maziko ambayo yatafanyika kesho kijijini hapo.
No comments:
Post a Comment