MATUKIO PICHA MKUTANO MKUU WA CCM UKIMCHAGUA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA HICHO UCHAGUZI MKUU 2020 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Saturday, 11 July 2020

MATUKIO PICHA MKUTANO MKUU WA CCM UKIMCHAGUA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA HICHO UCHAGUZI MKUU 2020

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi mara baada ya kuteuliwa kuwa Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika hapo badae mwaka huu.

Wajumbe Mbalimbali wa Mkutano Mkuu wa CCM wakishangilia wakati Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Conventional Center jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameketi pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa David Msuya wakati akisubiri kutangazwa kwa matokeo mara baada ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kumpigia kura.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipiga makofi pamoja na Wajumbe wengine walioshiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa wakati akisubiri matokeo mara baada ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu kupiga kura.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa anapiga makofi katika mkutano huo Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM ambao ulimchagua Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mgombea Urais katika Uchaguzi utakaofanyika baadae mwaka huu. Rais Dkt. Magufuli alimchagua tena Makamu wa Rais kuwa Mgombea Mwenza.
Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana akielekea jukwaa kuu kusalimia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijiji Dodoma Jumamosi Julai 11, 2020, ikiwa ni siku moja baada ya chama hicho tawala kumsamehe baada ya kuomba radhi kwa makosa aliyoyafanya miezi kadhaa iliyopita.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiondoka katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Conventional Center mara baada ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM uliompigia kura zote kwa ajili ya kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu. PICHA NA IKULU.
Kwaya ikitumbuiza wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijiji Dodoma Jumamosi Julai 11, 2020.

Wajumbe Mbalimbali wa Mkutano Mkuu wa CCM wakishangilia wakati Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Conventional Center jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment