MAKADA KIBAO WAJITOSA KUGOMBEA CCM, WAMO HASUNGA, BASHUNGWA,PROF KAPUYA.... - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 15 July 2020

MAKADA KIBAO WAJITOSA KUGOMBEA CCM, WAMO HASUNGA, BASHUNGWA,PROF KAPUYA....

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amechukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Julai 14, 2020. Anayemkabidhi fomu hiyo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nbozi Ndg Julius Mbwiga. (Picha Zote Na Mathias Canal)

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisalimiana na wanachama wa CCM waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu mara baada ya kuwasili katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbozi kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Julai 14, 2020. 

Mhe. Innocent Bashungwa akiwa kwenye Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Karagwe kuchukua fomu ya maombi ya kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Karagwe.

Mhe. Innocent Bashungwa akiwa kwenye Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Karagwe kuchukua fomu ya maombi ya kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Karagwe.


Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisalimia na kada wa CCM Ndg John Kihwele mara baada ya kuwasili katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbozi kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi leo Julai 14, 2020.

Katibu wa Kamati ya Maudhui, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Philip Filikunjombe akichukua fomu kuomba kuteuliwa kuwania jimbo la Ludewa.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mfanyabiashara, NAWAB MULLAH akichukua fomu kuwania ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM.
Prof. Juma Kapuya akichukua fomu kugombea Ubunge Jimbo la Kaliua.

MTIFUANO wa kugombea nafasi za ubunge na udiwani umeanza rasmi huku idadi kubwa ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakijitokeza kiasi kikubwa. Miongoni waliojitokeza wamo Mhe. Innocent Bashungwa akiwania Jimbo la Karagwe, Nawab Mullah akiwania Jimbo la Kawe, Japhet Hasunga anayeliomba Jimbo la Vwawa mkoani Songwe, pamoja na Dk. Philip Filikunjombe akichukua fomu kuomba kuteuliwa kuwania Jimbo la Ludewa. 

Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Shaibu Ngatiche anasema zaidi ya wanachama 203 hadi kufikia jana saa saba na nusu walikuwa wamejitosa kuchukua fomu za kuwania nafasi za ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa Mara.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Kigamboni, Evarist Mluge anawataja Winifrida Shonde, Frank Chalamila, Kassim Juma, Edwin Kweshijabo, Christian Hall, Daniel Sarungi, Ally Malima, Januari Kimanywa, Wande Kasaja, Kwesi Ukwaju, Dk. Faustine Ndungulile, Lilian Wassira, Eliudi Mganga pamoja na Sogone Wambura.

Anasema wengine waliojitokeza eneo hilo ni Mujuni Mwajauki (Mpoki), Christopher Sauti, Daniel Madushi, Deogratous Kanyesa, Ramadhan Abdallah, Emanuel Lyimo, Rajabu Gundumu, Buimura Mboja, Winifrida Shonde, Denis Kalikawe, Thaddeus Musembi, Themis Rwegasira, Rashid Jumbe
Ally Msaki, Francis Mugisha, Jovin Sanga, Fredrick Mumba, Dk. Benjamin Mohamed na Dorit Glorious.


Taarifa zinaeleza kuwa wagombea 57 wa CCM wamejitokeza kugombea ubunge na uwakilishi katika majimbo matano ya Wilaya ya Dimani Zanzibar, yaani wanaume 50 na wanawake 7. Majimbo wanayogombea ni pamoja na Dimani, Mwanakwerekwe, Fuoni, Pangawe na Kiembe Samaki.

No comments:

Post a Comment