PAZIA LA UCHUKUAJI FOMU BUKOBA, WAGOMBEA WAPIGANA VIKUMBO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 15 July 2020

PAZIA LA UCHUKUAJI FOMU BUKOBA, WAGOMBEA WAPIGANA VIKUMBO

Wakili msomi Aaroni Kabunga ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mawakili wa kujitegemea kanda ya Kagera kushoto akipokea fomu ya kugombea ubunge jimbo la Bukoba mjini kutoka kwa Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Bukoba mjini Ndg. Editha Domician kulia ambaye ni katibu wa vijana wilaya ya Bukoba mjini.

Mfanyabiashara maarufu Audax Kaijage Maarufu kama Omujumba kushoto akipokea fomu ya kugombea ubunge jimbo la Bukoba mjini kutoka kwa Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Bukoba mjini Ndg. Editha Domician kulia ambaye ni katibu wa vijana wilaya ya Bukoba mjini.

Ndg. Kilwanila Kiiza aliyekuwa katibu wa hospitali ya rufaa mkoa Kagera Bukoba akiwa ameshikilia fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Bukoba mjini baada yab kukabidhiwa na katibu.

Baadhi ya wagombe wa ubunge jimbo la Bukoba mjini wakisubiri kuingia katika ofisi ya katibu wa CCM wilaya Bukoba mjini kuchukua fomu. Picha zote na Allawi Kaboyo.
Na Allawi Kaboyo, Bukoba

BAADA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutangaza wagombea wake kwa nafasi za ubunge, udiwani na uwaakilishi kuanza kuchukua fomu tarehe 14 julai mwaka huu, hali katika ofisi za chama hicho manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera zimeonekana kufulika watia nia waliokuja kuchukua fomu kwaajili ya kuwania nafasi za ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini.

Miongoni mwa waliofika katika ofisi hizo na kuchukua fom ni wakili msomi Aaron Kabunga ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mawakili wa kujitegemea kanda ya Kagera ambaye amesema kuwa licha ya kuwa yeye ni wakili laki pia ni mwanachama hai wa chama hicho hivyo baada ya kujipima ameona anatosha kuwatumikia wanabukoba mjini kupitia ubunge.

Ameeleza kuwa msimu huu chama kimewapa nafasi kila mwananchama anayejua anatimiza vigezo kugombea nafasi yoyote ikiwa ni demoklasia hivyo ameona anayohaki ya kuchukua form na kugombea na matumaini yake ni kwamba chama kikimpitisha basi ataweza kuipeperusha vyema bendera katika uchaguzi mkuu.

“Nimefika hapa kuchukua fom kwaajili ya kuomba nafasi ndani ya chama change kuipeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya ubunge wa jimbo la Bukoba mjini, ni imaani yangu fomu hii nitaisoma na kuielewa na baadae nitaijaza na kuirudisha, lengo langu ni kuwatumikia watanzania wa Bukoba mjini hivyo nikishukuru chama kwa kutupa nafasi wanachama wote.” Amesema wakili Kabunga.

Kabunga amesema kuwa mambo ni mengi ya kuifanyia Bukoba ni mengi na anayo malengo makubwa kwaajili ya Bukoba kwakuwa kwa miaka mitano jimbo hilo lilikuwa upinzani na sasa ni muda wa kulikomboa.

Wengine waliochukua fomu ni mfanyabiashara maarufu Audax Kaijage maarufu Omujumba ambaye pia aliwahi kuwa diwani kwa kipindi kilichopita ambaye kasema kuwa lengo ni kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Bukoba mjini.

Bi Cristine Rwezahula ni mwanamke ambaye nay eye amejitosa katika kinyanganyiro cha kuwania kuipeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya ubunge jimbo la Bukoba mjini ambapo amesema kuwa anaamini chama kimewapa nafasi kubwa wananwake katika nafasi za utawala hivyo ameona anafaa kugombea ubunge katika jimbo hilo.

Ameongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa katika chama chao hivyo kama chama kimewaamini sasa hawana sababu za kusita kugombea nafasi za uongozi na kuwatumikia watanzania.

Mwingine ni aliyekuwa katibu wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Kagera Bukoba Ndg.Kilwanila Kiiza, Ndg. Valeriani Rugarabamu na wengine wengi ambao hadi saa saba mchana waliochukua fomu walikuwa wamefikia Zaidi ya wagombea 20 kwa jimbo la Bukoba mjini.

No comments:

Post a Comment