BENKI ya
CRDB imezindua huduma ya kukusanya maoni kwa wateja wake kupitia mfumo wa
kidijitali (QR Code) katika Jiji la Mwanza hatua itakayowarahisishia wateja
kutoa maoni na kuhudumiwa kwa wakati.
Uzinduzi wa
huduma hiyo ulifanyika Jumatatu Julai 13, 2020 katika benki ya CRDB tawi la
Mwanza ikiwa ni utekelezaji kwa vitendo kauli mbiu isemayo “TUNAKUSIKILIZA”
ambapo kwa mara ya kwanza nchini huduma hiyo ilizinduliwa mwezi Machi mwaka huu
jijini Dar es salaam.
Awali
kulikuwa na mzunguko mrefu kwa wateja kutoa maoni kupitia matawi ya CRDB tofauti
na mfumo huo mpya ambao popote mteja alipo anaweza kutumia simu janja yake na kuhudumiwa.
No comments:
Post a Comment