Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Iringa vijijini, Adestino Mwilinge akijitosa kugombea Jimbo la Isimani.
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
MBUNGE wa Jimbo la Isimani
William Lukuvu ameanza kupata upinzani katika jimbo hilo baada ya kada wa CCM, Adestino Mwilinge
kutangaza nia ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge jimboni humo.
Akizungumza na waandishi wa
habari katika Kijiji cha Mbuyuni kada huyo alisema ameamua kutia nia kwa
mujibu wa kanuni na katiba ya chama hicho inavyosema kila mwananchama anahaki
ya kuchaguliwa na kuchagua (ibara ya 14 (3) na 15 (1)).
Alisema kuwa ameamua kwenda kutia nia
akiwa kijijini kwao ili wadau watambue kuwa yeye ni mkazi halali wa Jimbo la
Isimani na anania ya dhati ya kusaidia
kuleta maendeleo kwa wananchi wanaishi katika jimbo hilo.
Mwilinge alisema ameamua kutia
nia baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Dk. Bashir Kakurwa
kutangaza wanachama wa chama hicho kuwa wanaruhusiwa kutia nia kwa sasa kwani ni wajibu
wao kulingana na katiba ya chama hicho.
Aliongeza kuwa anaunga mkono
juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe
Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuleta maendeleo ya nchi katika
kipindi hiki cha miaka mitano ikiwa madarakani.
Kada huyo aliyehudumu katika Chama Cha Mapinduzi kwa zaidi ya miaka kumi na tano akiwa katika uongozi wa
nyadhifa ndani ya chama chake.
Mwilinge alisema kwa sasa
hawezi kueleza sababu iliyomfanya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa
mgombea wa Jimbo la Ismani, japokuwa ameahidi kuweka wazi vipaumbele vyake muda
utakapofika.
Aidha Mwilinge alisema kuwa
wanachama wa CCM wanawajibu wa kukilinda chama hicho kwa
kuisimamia vizuri Serikali na kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na chama.
No comments:
Post a Comment