Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kulia akionyeshwa michoro mbalimbali ya kituo
cha Polisi cha zamani wilayani Pangani na Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani
(OCD) Georgina Matagi wakati alipokwenda kuwashukuru wasamaria wema wilayani
humo waliojitolea ujenzi wa kituo cha Polisi ili kutokomeza uhalifu.
Sehemu ya wadau wa maendeleo wilayani Pangani wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro.
Sehemu ya wadau wa maendeleo wilayani Pangani wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro.
MKUU
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kushoto akipata maelezo
mapokezi wakati alipoingia kwenye kituo cha Polisi Pangani akiwa na
kulia Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi na Katibu
Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akikitembelea Kituo cha
Polisi Pangani wakati alipokwenda kuwashukuru wasamaria kwa
kujitolea kufanikisha ujenzi wa kituo cha Polisi, kulia ni Mkuu wa Jeshi
la Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi.
MKUU wa Jeshi la
Polisi nchini IGP Simon Sirro amewapa mtihani wakuu wa Polisi wa wilaya nchini
(OCD) ambao watakutwa kwenye maeneo yao hawajafanya jambo lolote la kimaendeleo
atalazimika kuwaondoa kwa kuonekana kutokuwa na tija.
IGP Siro aliyasema
hayo wakati alipofika wilayani Pangani kwa lengo la kuwashukuru wasamaria waliojitolea kufanikisha ujenzi wa kituo cha Polisi wilayani humo juhudi
ambazo zimefanywa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo Georgina Matagi.
Alisema kwamba kazi
kubwa iliyofanywa na Mkuu huyo wa Polisi wilaya kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo inapaswa kuigwa na wakuu wengine hapa nchini huku akiwataka kuacha
kuwa watu wa kulialia bali wahakikishe wanakuwa wabunifu kwa kuiga mfano wa OCD
wa Pangani.
“Ma-OCD msiwe watu wa
kulia muwe wabunifu kuiga mfano wa Mkuu wa Polisi Pangani (OCD) huku akimtaka
kuendelea hivyo hivyo kwa sababu kwani kuna ma ocd mawe hawafikirii namna ya
kusaidia jeshi anachojua ni kumsubiri IGP ampelekee fedha…IGP yupo sawa, Amri
Jeshi Mkuu yupo, wewe ni ODC na RPC kuna vitu unaaweza kujiongeza kwa kuwatumia
wadau kuweza kusaidia,”Alisema IGP Siro.
“Lakini pia OCD
umenipa changamoto mimi niko smati sana sijua imekuwaje nikaisahau Pangani mpaka
wewe bwana mdogo ukaja kufanya hii kazi nzuri hongera sana kwa kazi kubwa na
nzuri ya kuhakikisha ujenzi huo unafanyika na kukamilika “Alisema.
Aidha aliwashukuru wadau
hao na OCD kwa kazi kubwa ya kulisaidia Jeshi la Polisi kujenga kituo
hicho huku akiwaambie kwamba walichokifanya
kwa faida ya watanzania wote kwa kuacha alama ya kesho na kesho kutwa haupo watu
watakukumbuka hivyo kwa niaba ya Rais niwashukur sana kwa kazi nzuri mliyofanya
kituo hiki huku nyuma hahakikuwa hivi msione mmepoteza bali mmeongeza fursa.
Hata hivyo alisema
kwamba kuna vitu ambavyo havijakamilika hivyo nitatoa milioni tano huku
akiwaomba wadau wa maendeleo nchi nzima walisaidie Jeshi la Polisi kwa sababu
usalama ndio kila kitu wanakwenda msikitini na kanisani kwa sababu ya usalama
na usipokuwepo ni hatari hivyo kila mtu ambaye mungu amemjalia kipato akiona
mahali kuna shida ya kituo cha Polisi asaidie,kwani vituo hivyo vitawasaidia.
Akizungumzia suala la amani na usalama IGP Siro alisema linaumuhim sana kwani likisha vurujika ni vigumu kuweza kurejesha huku akitolea mfano watu wa Msumbiji kwa sababu usalama haupo ni
mpakani wakati wa uchaguzi watu wenye
nia mbaya wanaweza kuleta mambo ya hovyo hovyo watoe taarifa wasimuamini kila
mtu ni vuzuri wakavijulisha vyombo vya ulinzi na usalama.
Alisema kwamba wakati
wa uchaguzi lolote linaweza kufanyika wabaya wetu wakachukua nafasi kufanya
mambo maovu wanaweza kuingia hivyo niwaombe mkiona ya namna hiyo hakikisheni
mnatoa taarifa kwenye vyombo vinavyohusika ili kuweza kufanyiwa kazi mambo
hayo.
Hata hivyo alisema usalama
watanzania walioukuta wajitahidi sana kuulinda huku akisema wachache wanaotaka
kuleta figisufigisu watahakikisha wanashughulikiwa na kurudishwa kwenye mstari.
No comments:
Post a Comment