IBADA YA KUMUAGA MKAPA TAIFA, BARAZA LA MAASKOFU LAMWELEZEA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Sunday, 26 July 2020

IBADA YA KUMUAGA MKAPA TAIFA, BARAZA LA MAASKOFU LAMWELEZEA...!

Gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba Jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati likiwasili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Ibada ya Kanisa Katoliki ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa ikiendelea katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Makanali wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati wakiingia katika sehemu ya Ibada katika Misa ya Dominika ya 17 ya Mwaka ‘A’ wa Kanisa Katoliki pamoja na Kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba Jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati likiwasili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Makanali wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati wakiingia katika sehemu ya Ibada katika Misa ya Dominika ya 17 ya Mwaka ‘A’ wa Kanisa Katoliki pamoja na Kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Msafara wa mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa ukiwasili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba Jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati likiwasili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa Mama Anna Mkapa akiwa pamoja na familia yake katika Misa hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa Mama Anna Mkapa akiwa pamoja na familia yake katika Misa hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa wakishiriki Misa ya Dominika ya 17 ya Mwaka ‘A’ wa Kanisa Katoliki pamoja na Kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Na Joachim Mushi, Dar

IBADA maalum ya kumuombea Hayati Rais Mstaafu Benjamin Mkapa imefanyika Uwanja wa Taifa Uhuru jijini Dar es Salaam huku Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) likimuelezea kiongozi huyo alikuwa mwema na mwenye upendo kwa watu wote Watanzania na Waafrika kwa ujumla.

Ibada hiyo iliyoongozwa na Muhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwe na kusaidiwa na maaskofu, Agapiti Ndorobo wa Jimbo la Mahenge, Antony Banzi wa Jimbo Tanga na askofu Alfred Maluma wa Jimbo la Njombe imehudhuriwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi pamoja na wananchi na viongozi mbalimbali.

Wakitoa neno katika ibada hiyo takatifu, TEC ilisema Hayati Mkapa alikuwa mtu wa pekee kwani aliweza kusikiliza shida ya kila mmoja aliyemfuata kuomba ushauri na kumsaidia kadri ya uwezo wake, alikuwa na hekima na msikivu kwa wengine. Aidha TEC ilisema aliweza kuhudhuria mialiko mbalimbali ya kuchangia shughuli za ujenzi wa shule na hata nyumba za ibada jambo ambalo wanamshukuru Mungu kwa uwepo wa kiongozi huyo.

Aliwaomba wananchi wote kwa pamoja kumuombea Hayati Mkapa na kuendelea kuiombea na kuifariji familia yake wakati huu mgumu wa msiba ambao wapo kwenye majonzi makubwa. Alisema kuondoka kwa Hayati Mkapa ni pengo kubwa kwa taifa hivyo kila mmoja anakila sababu za kumuombea kiongozi huyo.

Mwili wa Hayati Benjamin Mkapa kabla ya kuwasili Uwanja wa Uhuru ukitokea Hospitali ya Lugalo ulipita katika barabara kadhaa ukiagwa na wananchi waliojitokeza barabarani ikiwa ni kuonesha kuguswa na kifo cha kiongozi huyo wa taifa.

Baada ya kumalizika kwa ibada hiyo wananchi waliojitokeza wameanza kutoa heshima za mwisho uwanjani hapo katika eneo maalum lililojengwa na kuwekwa mwili huo ili kuwawezesha waombolezaji kuuaga kabla ya kusafirishwa hapo baadaye kuelekea mkoani Mtwara, kijijini Lupaso kwa ajili ya mazishi.

Zoezi la kutoa heshima za mwisho za kiongozi huyo litafanyika kwa siku tatu Uwanja wa Uhuru kuanzia leo kabla ya kusafirishwa kuelekea Mkoa wa Mtwara vijijini kwa mazishi ya heshima nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment