ABIRIA 40 WANUSURIKA KUFA KATIKA AJALI YA BASI MKOANI SINGIDA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 6 July 2020

ABIRIA 40 WANUSURIKA KUFA KATIKA AJALI YA BASI MKOANI SINGIDA

 Basi la Big  Nation lenye namba T 721 DEN kutoka Dar es Salam kwenda Kahama Shinyanga likiwa limepata ajali mjini Singida.

 Abiria aliyenusurika katika ajali hiyo, Juma Julius akizungumzia ajali hiyo.

 Basi la Big  Nation lenye namba T 721 DEN kutoka Dar es Salam kwenda Kahama Shinyanga likiwa limepata ajali leo mjini Singida.

Majeruhi wa ajali hiyo wakipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.


Na Dotto Mwaibale, Singida

WATUA 40 waliokuwa wakisafiri kwa Basi la Big  Nation lenye namba T 721 DEN kutoka Dar es Salam kwenda Kahama Shinyanga wamenusurika kufa  baada ya kupata  ajali katika eneo la Mizani nje kidogo ya mji wa Singida baada ya kuligonga kwa nyuma Lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T981 DER.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya basi hilo  kukosa mwelekeo na kwenda kutumbukia darajani kwa kile kinachodaiwa kuwa dereva alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Deogratius Banuba amekiri kupokea majeruhi watano ambao wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuendelea vizuri.

Baadhi abiria ambao walikuwa wanasafiri na basi hilo walisema kuwa licha ya kulalamikia ubovu wa basi hilo ambalo wamedai limeharibika mara kadhaa njiani lakini wahusika hawakujali.

" Basi ili lilikuwa likiharibika mara kwa mara njiani lakini hata tulipo lalamika watubadilishie jingine hawakukubali" alisema mmoja wa abiria aliyenusurika katika hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Juma Julius.

Abiria hao wakiwa eneo la ajali wameomba Serikali mkoani hapa  kuwatafutia usafiri mwingine baada ya kukaa kwa masaa zaidi ya manne bila kupata usafiri mwingine.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida ili kuzungumzia ajali hiyo hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu yake mara kadhaa bila ya kupokelewa.

No comments:

Post a Comment