RC BYAKANWA AIPONGEZA NANYUMBU KUPATA HATI SAFI MFULULIZO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 4 June 2020

RC BYAKANWA AIPONGEZA NANYUMBU KUPATA HATI SAFI MFULULIZO

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius G. Byakanwa akizingumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, Ndg. Hamis H. Dambaya akizungumza katika Baraza hilo.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Nanyumbu imepongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa kupata hati Safi kwa miaka minne mfululizo.

Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Nanyumbu, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa pongezi za dhati kwa Halmashauri hiyo kwa kuendelea kufanya vizuri katika matumizi ya fedha.

Mkuu wa Mkoa pamoja na pongezi hizo, ameitaka Halmashauri kuhakikisha inazishirikisha Taasisi zingine ikiwemo TAKUKURU pindi inapokuwa na miradi mikubwa ili kuepuka hoja za ukaguzi. Aidha, Mhe. Byakanwa ameagiza Halmashauri kuhakikisha inakusanya madeni kwa wakati toka vikundi vinavyokopeshwa fedha za mfuko wa Wanawake, vijana na walemavu.

Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zinazoishia Juni 30, 2019, inaitaja Halmashauri hiyo kuwa iliandaa hesabu zake kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya ufungaji wa hesabu kwa taasisi za Umma (IPSAS) na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imetolewa na; Ofisi ya Habari,
NANYUMBU.

No comments:

Post a Comment