MAZISHI YA MPIGA PICHA WA WAZIRI MKUU, MFINANGA…! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 4 June 2020

MAZISHI YA MPIGA PICHA WA WAZIRI MKUU, MFINANGA…!

Padre Japhet Njaule wa parokia ya Vuchama akipanda msalaba kweye kaburi la aliyekuwa mpigapicha wa Waziri Mkuu, Bw. Christopher Mfinanga wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana Juni 3, 2020 katika makaburi ya familia kijijini Mangio, Vuchama, wilayani Mwanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Jeneza lenye mwili wa Christopher Mfinanga likiwa kaburini wakati wa mazishi yaliyofanyika jana Juni 3, 2020 katika makaburi ya familia kijijini Mangio, Vuchama, wilayani Mwanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Tom Apson akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa mpigapicha wa Waziri Mkuu, Bw. Christopher Mfinanga wakati wa mazishi yaliyofanyika jana Juni 3, 2020 katika makaburi ya familia kijijini Mangio, Vuchama, wilayani Mwanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Wachungaji na Padri walioshirikiana kuongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mpigapicha wa Waziri Mkuu, Bw. Christopher Mfinanga wakichukua udongo ili wauweke kaburini kwenye mazishi yaliyofanyika jana Juni 3, 2020 katika makaburi ya familia kijijini Mangio, Vuchama, wilayani Mwanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mama mzazi wa aliyekuwa mpigapicha wa Waziri Mkuu, Bw. Christopher Mfinanga akipita kuaga mwili wa mwanaye wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika jana Juni 3, 2020 kijijini Mangio, Vuchama, wilayani Mwanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mama mzazi wa Christopher Mfinanga akiweka shada la maua wakati wa mazishi yaliyofanyika jana Juni 3, 2020 katika makaburi ya familia kijijini Mangio, Vuchama, wilayani Mwanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mchungaji Bill Grahama Msangi wa KKKT Usharika wa Vuchama akihitimisha ibada ya mazishi ya aliyekuwa mpigapicha wa Waziri Mkuu, Bw. Christopher Mfinanga wakati wa mazishi yaliyofanyika jana Juni 3, 2020 katika makaburi ya familia kijijini Mangio, Vuchama, wilayani Mwanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Makaburi mawili, moja la Baba na jingine la mwana. Kulia mbele ni kaburi la aliyekuwa mpigapicha wa Waziri Mkuu, Bw. Christopher Mfinanga na la kushoto ni la Baba yake Mzee Edward Dologha Mfinanga aliyefariki jijini Arusha Mei 19, 2020 na kuzikwa Mei 21, 2020 kijijini kwake Mangio, Vuchama, wilayani Mwanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment