LUKUVI AWATAKA WATENDAJI IDARA ZA ARDHI KUPIMIA WANANCHI ARDHI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 25 June 2020

LUKUVI AWATAKA WATENDAJI IDARA ZA ARDHI KUPIMIA WANANCHI ARDHI

Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi akiwasili kwenye uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi mkoa wa Arusha mapema leo akiwa maeongozana na mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta pamoja na katibu tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega nyuma wakiwa na mkuu wa wilaya ya Monduli Edward Balele picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Na Ahmed Mahmoud Arusha

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Makazi, William Lukuvi amewataka maafisa ardhi kuwapa hati Mara moja watu wote waliopimiwa viwanja ili idadi iliyo kwenye michoro iwe na hati kwa ajili ya kuondoa migogoro.

Aidha aliwataka watu wote walio mjini kuanza kuchukuwa hati za nyumba zao ili  uondokana na ulofa ambapo watambue kuwa hakuna makazi holela na wanaosema hivyo wanawanyima umiliki wa Ardhi kwa faida ya maisha yao na kwamba hati hizo huwasaidia kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha.

Aliyasema hayo wakati akizindua ofisi ya Ardhi mkoa wa Arusha zilizopo kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha nakuwataka kuacha madalali wa Ardhi kutumia ofisi za ardhi na kuwatapeli wananchi.

Alisema kuwa hataki makandokando kwenye ofisi za ardhi kwani Kuna baadhi ya maafisa huwatumia makanjanja kutoa taarifa za ardhi wakiwa Chini ya mti na baadaye haohao ndio hutumika kuwakusanyia fedha.

Mkurugenzi wa jiji la Arusha ametakiwa kufanya tathmini ya Watendaji wake ili kubaini ambao hawatendi haki na wajibu wao ili  kuwaondoa Mara moja na kuchagua wengine ambao wataweza kwenda na kasi ya awamu ya tano.

Hata hivyo ameweza kumfukuza kazi afisa ardhi aliewahi kufanya kazi katika halmashauri ya Meru Nicodemas Hiru kwa kitendo Cha kumpa ardhi yenye hekari 3000 na kuingizia serikali asara ya shilingi milioni miatano kwa kulipa fidia  wakati huo huo alimpandisha cheo  aliekuwa afisa ardhi halmashauri ya Arusha ,nakumfanya kuwa afisa ardhi katika
jiji la Arusha Rehema  Jato.

Lukuvi akiongelea swala la kiwanja Cha ujenzi wa Standi eneo la Bondeni Seed kilichokuwa na mgogoro muda mrefu na hati yake ilikuwa haionekani  alisema kuwa hati ya eneo hilo anayo na Mkurugenzi nenda kwa kamishna wa Ardhi mkoa akupe ili kuondoa changamoto hiyo.

"Hati ya kiwanja cha Bondeni Seed ninayo mimi Mkurugenzi wa Halmashauri ondoa hofu kwani mgogoro umeshakwisha wewe jipange kumaliza kazi uliyoagizwa na Mh.Rais ya ujenzi wa Standi na kama kuna mtendaji wa idara ya Ardhi haiendani na kasi ya awamu ya tano huyo kashughulike naye kwani kumekuwa na changamoto kubwa kwenye idara hiyo
jiji la arusha nami najua"

"Mkurugenzi wa jiji nakupa hati ujenge Standi katika eneo la Bondeni city  eneo Hilo hutalipia fidia Wala kulipiana fedha za kujenga Standi hiyo utazipata tu "alibainisha Lukuvi

Aidha alisema kuwa kumekuwa na makandokando mengi kwenye Idara ya Ardhi jiji la Arusha ikiwemo ya kufanyakazi na matapeli ambao wamekuwa kwenye magari wakipanga mipango ya kuzulumu wananchi hivyo kumtaka mkurugenzi mpya kuwa macho akibaini kumpa taarifa maepema ili ashughulike nao.

Alibainisha kuwa Hati mia mbili anazotoa leo ziwe chachu ya kuimarisha uchumi kwa wananchi na watendaji wa idara za Ardhi kuacha kutumia vibaya ofisi kwani ofisa wa Ardhi atakayebainika kwenda kinyume na maagizo ya serikali wasisiste kumchukulia hatua.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta alisema kuwa ofisi ya Ardhi kumekuwa na changamoto nyingi ikiwepo ya eneo la ofisi kwa ajili ya kuhifadhia taarifa za wananchi hivyo aliwahaidi Ndani ya wiki moja atakuwa amewapatia eneo ambapo alimuagiza katibu Tawala mkoa wa Arusha kupitia viwanja vyake na Hadi ifikapo ijumaa awe ameshampatia eneo.

Alisema kuwa kwa sasa yupo tayari kufanya kazi na mwananchi yeyote ambaye anakero aipeleke ofisini kwakwe siku yoyote atazitatua na hata weka siku ya kusikiliza kero hizo Bali mwananchi yeyote mwenye shida aipeleke mkoani,huku aliwataka Watendaji wa serikali kubadilika.

Kwa Upande wake mkuu mpya wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosa alimshukuru mh.Rais kwa kumteua kuwa mkuu wa wilaya hiyo na kuahidi utumishi uliotukuka kwa wananchi wa wilaya ya Arusha huku akiwataka kumpa ushirikiano pamoja na mshikamaono kwa kutanguliza maslahi mapana kwa nchi na wilaya.

No comments:

Post a Comment