Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Makala Mapesah akizungumzia msaada wa ndoo maalum za kusaidia kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Makala Mapesah akionyesha ndoo maalum za msaada kwa ajili ya wananchi kujitakasa na kujikinga na virusi vya Corona
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi
(UVCCM) Wilaya ya Iringa vijijini umeeleza kuwa zoezi la uelimishaji jamii
pamoja na ugawaji wa vifaa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya
corona ni zoezi endelevu wanalolitekeleza kwa sasa ili kuiepusha jamii na
maambuzi.
Akizungumza na blog hii Mwenyekiti
wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Makala Mapesah
alisema kuwa tangu ilipogindulika kuwapo kwa maambukizi ya Virusi vya Corona
nchini UVCCM walianzisha mkakati maalum wa uelimishaji jamii katika vijiji vyote
vya wilayani humo sambamba na ugawaji wa
vifaa ikiwemo ndoo za maji na sabuni ili kuwawezesha kutajitakasa kama
inavyoelekezwa na wataalam wa afya.
Makala alisema kuwa kando ya
kuifikia jamii moja kwa moja kwa namna salama ya kujikinga na maambukizi pia wamekuwa wakitumia vyombo vya habari ikiwemo Radio,Runinga, vipeperushi, magazeti na
mitandao ya kijamii kwa lengo la kuhakikisha kila mmoja anafikiwa na elimu
sahihi na kuepuka maambikizi vya virusi vya Corona vinavysababisha ugonjwa wa
Covid 19.
Alisema kuwa wamefanikiwa kutoa
msaada wa ndoo maalum za kutakasia mikono,vitakasa mikono na Barakola kwa
wananchi katika vijiji vyote ili waendeleee kujikinga dhidi ya maambukizi ya
virusi hivyo vinavyohatarisha maisha ya
binadamu duniani kote.
“Tumefanikiwa kutoa elimu hii
kwa ushirikiano wa ofisi za serikali,viongozi wa chama cha Mapinduzi mkoa na
wilaya ya Iringa,wabunge na wadau mbalimbali ambao walifanikisha kuwafikia
wananchi kwa kutoa elimu na misaada mbalimbali ya kujikinga na kupambana na
virusi vya Corona” alisema Makala.
Aliwaomba wadau na viongozi
mbalimbali kuendelea kutoa elimu ya kupambana na virusi vya Corona hasa
vijijini kwa kuwa bado hawana elimu ya kutosha juu ya vurusi hivyo pamoja
changamoto ya kupatikana kwa Barakola limekuwa tatizo kwa wananchi hasa wa
maeneo hayo.
Aidha Mwenyekiti wa umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Makala Mapesah sambamba
na hayo alizungumzia kuhusu changamoto inayowakabili wakazi wa kijiji cha Isele
kitongoji cha Mbingama waliokumbwa na mafuriko katika mvua za msimu huu na
kueleza kuwa wanaendelea kuwafikishia misaada ya hali na mali ikiwemo
inayotolewa na wadau wa chama cha mapinduzi wakiwemo viongozi wa chama hicho
tawala nchini
Alisema Umoja wa Vijana wa Chama
cha Mapinduzi Wilaya ya iringa walifanikiwa kuwatafutia Chakula,Nguo,Makazi na
pamoja na baadhi ya vifaa tiba ili kuongeza hamasa kwa wataalam wa afya
kuendelea kuwahudumia kwa ufanisi wananchi hao kwa kushirikiana na serikali ya
Wilaya ya Iringa.
“Tunapenda kumshukuru mkuu wa
Wilaya ya Iringa Richard Kasesela na viongozi wake kwa kuwatafutia makazi mapya
wananchi waliokuwa wamekubwa na mafuriko katika kitongoji cha Mbingama” alisema
Makala
Makala katika hatua nyingine
aliipongeza kampuni ya QWIHAYA kwa msaada walioutoa kwa wananchi waliokumbwa na
mafuriko katika Kijitongoji cha Mbingama kijiji cha Isele tarafa ya Pawaga na
kuongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa mdau mkubwa hasa kwenye utatuzi wa
changamoto zinazowakabili wananchi katika kipindi cha majanga, mbalimbali
ikiwemo mafuriko na janga hili la sasa la maambukizi ya corona nchini.
“Kampuni ya QWIHAYA imesaidia sana
hata kwenye kujikinga na maambukizi ya kupambana na virusi vya Corona kwa kutoa
msaada wa vifaa vya kijikinga na virusi hivyo mkoani Iringa na Tanzania kwa
ujumla” Alisema Makala
Mwenyekiti huyo wa UVCCM
Wilayani Iringa Mkala Mapesah alizihimiza kampuni zingine za mkoani Iringa na
Nje ya Iringa pamoja na wadau wa maendeleo kwa ujumla kuiga mfano wa Kampuni ya
QWIHAYA kwa kuendela kushirikiana na Serikali ya chama cha Mapinduzi katika
kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii katika kipindi
hiki cha maambukizi ya virusi vya corona
No comments:
Post a Comment