Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd, Ndugu Leonard Mahenda alikabidhi kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi vya corona Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium mbele ya mkurugenzi wa Mji wa Mafinga.
Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd, Ndugu Leonard Mahenda alikabidhi kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi vya corona Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium.
Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd, Ndugu Leonard Mahenda na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa halmashauri ya Mji wa Mafinga.
NA MWANDISHI WETU,MUFINDI.
BAADA ya kupokea mashuka 120 kutoka katika kampuni
ya Qwihaya General Enterprises Ltd, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium
ameishukuru kampuni hiyo na kuwaomba wadau wengine kuunga mkono jitihada
za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Covid 19.
Jana Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd,
Ndugu Leonard Mahenda alikabidhi kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi vya
corona.
Mbali na msaada huyo, kampuni hiyo imefanikiwa
kuikabidhi Serikali ya mkoa wa Iringa, vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh10
milioni yakiwemo mavazi 20 ya madaktari, matenki 60 ya kuhifadhia maji, barakoa
na vitakasa mikono.
“Kipekee nimshukuru ndugu yetu Qwihaya kwa
msaada huu, mashuka haya yatatusaidia, wito wangu kwa wadau wengine tuungane
mkono ili tuweze wote kwa pamoja kulikabili janga hili,” amesema DC wa Mufindi.
Awali, Ndugu Mahenda alisema bado kuna vifaa
vingine vimeandaliwa kwa ajili ya kuikabidhi wilaya hiyo katika kuendeleza
mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
“Bado tuna vifaa ambavyo tumeandaa kwa ajili
ya halmashauri yetu ambavyo tutaleta kuendelea kukabiliana na ugonjwa huu,
niwaombe wadau wengine waweze kujitokeza kukabiliana na ugonjwa huu,” amesema
Mahenda.
No comments:
Post a Comment