Mwanahabari Eliya Mbonea (kushoto) akishiriki tendo la kuchangia damu enzi zauhai wake. |
MWANDISHI wa Habari wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd inayochapisha Magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na Dimba pamoja na Mtanzania Digital, Bw. Eliya Mbonea amefariki dunia Jumatatu ya Aprili 6,2020 wakati akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (Arusha Press Club), Claude Gwandu amethibitisha taarifa za kifo cha Eliya Mbonea alipozungumza na mwandishi wa habari hii.
"Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) kinasikitika kutangaza kifo cha mwanachama wake, Eliya Mbonea kilichotokea Aprili 6 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili," alisema Gwandu.
Amesema Mbonea ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa APC kuanzia 2010 hadi 2013 alihamishiwa Muhimbili wiki tatu zilizopita kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC mjini Moshi ambako alikuwa akipatiwa matibabu tangu Februari 19, mwaka huu.
"Mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa Arusha na taarifa zaidi zitatolewa baada ya kukutana na familia yake....," amesema Gwandu.
No comments:
Post a Comment