MAAMBUKIZI YA CORONA NCHINI KENYA YAFIKIA WATU 142 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 6 April 2020

MAAMBUKIZI YA CORONA NCHINI KENYA YAFIKIA WATU 142

Upimaji virusi vya Corona Kenya.

KENYA
imethibitisha kuwa na wagonjwa wapya 16 wa corona, baada ya kuwafanyia vipimo watu 530. Hadi sasa Kenya imefikisha idadi ya watu 142 wenye maambukizi ya Corona.

Wizara ya afya nchini Kenya imetaarifu kuwa katika visa vipya 16, raia wa Kenya ni 15 na mmoja anatokea Nigeria. Raia 11 kati ya hao wana historia ya kusafiri nje ya nchi ilihali 5 ni raia wa eneo.

Watu 12 ni kutoka mji mkuu wa Kenya Nairobi, wengine watatu wanaishi Mombasa 3 na mmoja kutoka Kilifi. Waliokutwa na maambukizi mapya ni wennye umri kati ya miaka 22 na 66, wanaume ni tisa na wanawake saba.

Kati ya waliothibitishwa, tisa walikuwa kwenye karantini tayari. Wizara ya afya pia imeweka wazi kwamba inatengeneza barakoa ambazo zitasambazwa kwa wananchi hivi karibuni.

Wizara ya afya imeeleza kuwa watu watakaokufa kutokana na virusi vya Corona watazikwa ndani ya saa 24 huku watu wa karibu wa familia wasiozidi 15 wakiruhusiwa kuhudhuria mazishi hayo yatakayoandaliwa na Serikali.

Aidha, ndege kutoka nchi za kigeni zimeendelea kipigwa marufuku kuingia Kenya kwa siku 30 zaidi.

Hatahivyo, marufuku hii imeondolewa kwa ndege za kigeni zinazokuja kuhamisha raia wa nchi za nje waliokwama ingawa zinatakiwa kutoa taarifa kwa serikali angalau saa 72 kabla.

Ndege zingine ambazo hazitaathirika na marufuku hii ni zile za kubeba mizogo hasa ikizingatiwa kwamba kwa sasa serikali inaagiza vifaa vya wahudumu wa afya kutoka nje. Sekta ya uchukuzi pia imeagizwa kutekeleza sheria zilizotolewa.

Na kutokana na ongezeko hilo, kuanzia Jumatatu, matatu au daladala pamoja na bodaboda ambazo zitakiuka sheria zilizowekwa zitapokonywa leseni na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kusambaza virusi kimaksudi.
-BBC

No comments:

Post a Comment