Wafanyabiashara wa nyama Mkoa wa Singida wakiingiza kitoweo hicho katika maduka ya nyama yaliyopo Soko Kuu la Singida.
Mwonekano wa maduka ya nyama Soko Kuu la Singida.
Afisa Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Singida, Adranus Kalekezi (kulia) akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bravo Lyapembile kuhusu ukarabati wa machinjio ya nyama ya manispaa hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bravo Lyapembile akikagua ukarabati wa machinjio ya nyama ya manispaa hiyo.
Na Ismail Luhamba,Singida.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Singida, Bravo Lyapembile amewaondoa wasiwasi wachinjaji na wananchi kwa ujumla wanaozunguka machinjio ya manispaa hiyo iliyofungwa kwa muda na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) baada ya kuwepo na mapungufu yaliyosababishwa na mvua.
Mkurugenzi huyo alitoa rai hiyo na kuomba radhi kwa usumbufu uliyojitokeza kutokana na kufungwa machinjio hiyo baada ya kutembelea machinjio hayo ili kujionea hatua zilizofikiwa za ukarabati,kwa lengo la kuharakisha huduma za upatikanaji wa kitoeo cha nyama kwa wananchi wa manispaa na mkoa kwa ujumla
"Kwa sasa huduma ya uchinjaji inapatikana katika machinjio ya Mwankoko, Manga, Mtamaa pamoja na eneo la Mnada wa Kidikunku, hivyo wananchi wasiwe na shaka katika upatikanaji wa nyama wataendelea kupata huduma hiyo kama kawaida," alisema Bravo.
Licha ya Halmashauri hiyo kutenga maeneo mengine kwa ajili ya shughuli za uchinjaji wafanyabiashara hao wameilalamikia Manispaa hiyo kutokana na maeneo hayo kukosa huduma muhimu ikiwemo za maji safi na salama ambapo wanatumia gharama kubwa kufuata huduma hiyo ya maji safi na salama.
Mwenyekiti wa Wachinjaji Manispaa ya Singida, Jumanne Athuman alisema toka kufungwa kwa machinjio hiyo wamekuwa wakilazimika kuchinja na kuandaa nyama kwenye maeneo hayo yaliyotengwa na Manispaa ambayo yana changamoto.
Kwa mfano katika eneo la Mnada wa Kidikunku ambalo ndio tunalitumia kwa sasa kwa shughuli zote za uandaaji wa kitoweo cha nyama ,eneo hili halina huduma ya maji safi hivyo inatulazimu kubeba maji kutoka huku mjini ili tukaandae nyama hizo katika mazingira mazuri.”alisema mwenyekiti huyo na kuongeza:
"Hata hivyo mkurugenzi huyo aliwaomba wachinjaji hao waliohamishwa na kupelekwa maeneo mengine mbadala baada ya kufungwa machinjio hiyo kuzingatia usafi kwa kuhakikisha maeneo waliopangiwa kuchinja kwa muda yanakuwa masafi ili kuepushasha magonjwa yanayotokana na uchafu".
Aidha Bravo alisema Halmashauri hiyo imejipanga kujenga machinjio nyingine ya kisasa katika eneo la Ng’aida nje kidogo ya mji huo ambapo taratibu zote zimeshakamilika na ujenzi huo unatarajiwa kugharimu zaidi ya sh. bilioni tatu hadi kukamilika kwake.
Aidha mkurugenzi alisema tayari manispaa imekwishapata eneo katika Kijiji cha Ng’aida Kata ya Kisaki na tumeshafanya upembuzi yakinifu na michoro imeshakamilika, na kwamba kwenye machinjio hiyo ya kisasa wanatarajia kuweka kiwanda cha kusindika ngozi
No comments:
Post a Comment