KATIBU MKUU MWAKALINGA AKAGUA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA WIZARA KUJIKINGA NA CORONA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 14 April 2020

KATIBU MKUU MWAKALINGA AKAGUA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA WIZARA KUJIKINGA NA CORONA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, akihakiki utekelezaji wa mkakati wa Sekta ya Ujenzi kwa watumishi katika kutekeleza maelekezo ya Wizara ya Afya namna ya kujikinga na maambukizi ya Homa ya Mapafu (Covid  - 19), jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, akifafanua jambo kwa Mhasibu wa Sekta hiyo, Bw. Thomas Malima, namna ya utekelezaji wa mkakati wa Sekta ya Ujenzi katika kutekeleza maelekezo ya Wizara ya Afya namna ya kujikinga na maambukizi ya Homa ya Mapafu (Covid  - 19), jijini Dodoma.

Mhasibu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bw. Erick Lengama, akimuonesha Katibu Mkuu wa Sekta hiyo, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, namna ya kutumia kitakasa mkono katika shughuli zake za kila siku ofisini kwake, jijini Dodoma. Zoezi hilo ni hatua ya utekelezaji wa maelekezo ya Wizara ya Afya namna ya kujikinga na maambukizi ya Homa ya Mapafu (Covid  - 19).

Afisa Habari Mwandamizi, Bw. Shukuru Senkondo kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), akinawa mikono katika maji tiririka ikiwa ni utaratibu wa Sekta hiyo katika utekelezaji wa maelekezo ya Wizara ya Afya namna ya kujikinga na maambukizi ya Homa ya Mapafu (Covid  - 19), jijini Dodoma.

Mtumishi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Placidia Fabian, akimuonesha Katibu Mkuu wa Sekta hiyo, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, kitakasa mikono alichogawiwa na Sekta hiyo ikiwa ni hatua mojawapo ya kutekeleza maelekezo ya Wizara ya Afya namna ya kujikinga na maambukizi ya Homa ya Mapafu (Covid  - 19), jijini Dodoma. Katibu Mkuu huyo amefanya ziara ya kushtukiza kwa watumishi wake leo kubaini matumizi sahihi ya vitakasa mikono.

No comments:

Post a Comment