Wana kikundi cha coronadamas |
KAZI yao ni ya kupigiwa mfano lakini wakati huohuo inatia hofu: wanaosha miili ya waliokufa kwa vorusi vya corona. Watu waliojitolea kuosha maiti maarufu kama "coronadamas" wanaendesha kazi yao katika mji wa Iran wa Qom ili kutimiza moja ya tamaduni za tangu jadi ya dini ya Kiislamu ya kumuosha maiti kabla ya kuzikwa.
Iran ina idadi kubwa ya vifo vya wagonjwa wa corona Mashariki ya Kati. Ni vigumu sana kupata taarifa za uhakika ya kile kinachotokea lakini wachapishaji wengi wa vitabu wanasema kwamba hifadhi za maiti zimejaa.
Uwepo wa" coronadamas " kulijulikana kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo miili ya waliokufa ilionekana ikiwa imepangwa kwenye sakafu ikisubiri kuoshwa. Mwanamume aliyerekodi video hiyo alidai kwamba baadhi ya miili imekuwa hapo kwa siku 5 au 6.
Maswali yaliyoibuka kwenye mitandao ya kijamii yalisababisha mamlaka kuanza kudhibiti tukio hilo na kwanza mwanamume huyo alikamatwa lakini serikali ilitafuta mikakati ya kutuliza umma. Na hilo pia lilisababishwa maswali kuibika zaidi baada ya kusemekana kwamba waathirika wa covid-19 hawakupata mazishi yanayostahili kitu ambacho ni cha msingi katika dini ya Kiislamu.
Ni wakati huo ambapo mamlaka ilianza mazungumzo rasmi kuhusu watu hao waliojitolea kuosha maiti maarufu kama "coronadamas", kama namna moja ya kuhakikishia raia wake wapendwa wao wanaokufa kwa virusi vya corona wanazikwa kwa misingi ya dini ya Kiislamu.
Picha ya waoshaji hao wa maiti kisha ikaonekana katika tovuti za serikali zikionesha wanawake hao jasiri wanaohakikisha kwamba waliokufa wanazikwa kwa utaratibu wa dini ya Kiislamu tukio linalofahamika kama Ghusi.
Chini ya sheria za Kiislamum waliokufa wanastahili kuzikwa muda mfupi baada ya kufa. Lakini hilo kufanyika ni lazima mwili uoshwe kwa kuzingatia dini ya Kiislamu ambapo maiti huoshwa mara tatu kwa kufuata taratibu maalum.
Mara ya kwanza, maji yanatiwa mafuta ya mwerezi (cedar) mara ya pili anaoshwa na mafuta kafuri (camphor) na hatimae mwili huo unaoshwa na maji ya kawaida yanayotiririka. Kisha mwili unafunikwa nguo nyeupe maarufu kama sanda na mwili huo utakuwa tayari kufanyiwa sala ya mwisho na kwenda kuzikwa.
Lakini mchakato huo ni salama vipi iwapo mtu amekufa kwa ugonjwa wa covid-19? Janga hilo lilipoanza, kulizuka mkanganyiko kuhusu jinsi maiti inavyostahili kuoshwa kwa ngazi ya kimataifa na hata ndani ya Iran kwenyewe.
Awali, serikali ilishauri kutoosha maiti kwa maji, na kupendekeza uoshaji wa bila kutumia maji ambayo pia inaruhusiwa.
Mapema Machi, kiongozi mkuu wa kidini alitangaza kwamba maiti za waliokufa na covid-19 zioshwe kama inavyotakikana kwa kuzingatia utamaduni ambao umekuwepo, kuoshwa, kuvishwa sanda na kuswaliwa kabla ya kuzikwa.
Hatahivyo, aliongeza kwamba wale wanaofanya kazi hiyo wafuate kanuni na mwongozo wa shirika la afya duniani WHO.
Mwongozo
Wakati ambapo haijathibishwa kuwa virusi vya corona vinaweza kusambazwa kupitia maiti, Shirika la Afya Dunia (WHO) linashauri kuchukuwa tahadhari ya juu kwasababu viini vinavyosababisha ugonjwa huo havijulikani. WHO inapendekeza kuwa wale wanaotaka kushika maiti wavae mavazi kamili ya kujikinga ikiwemo glavu na barakoa.
Kwa mfano Italia, mamlaka za Afya zasema kwamba ingawa maiti haiwezi kusambaza virusi, vinaweza kuwa viko hai kwenye nguo, na hivyobasi, mara moja majeneza hufungwa na familia zikakatazwa kumuona mpendwa wao kwa mara ya mwisho.
Licha ya hatari zisizofahamika, nchini Iran wanaoosha maiti wanaendelea kufanya kazi kwa saa 24. Kuna timu tatu zinazofanyakazi kwa zamu ya saa saba ili kujaribu kuingilia namahitaji ya huduma hiyo. Wanawake wanaimba nyimbo za kujifariji wakati wanafanya kazi hiyo.
Lakini sio wao peke yao wanaofanya kazi hiyo: katika eneo la Mashhad, wanafunzi pia huosha maiti wakati wa chakula cha mchana. Kuchelewa kuosha maiti sio tu ni kwasababu ya uwoga wa wanaoishi maiti lakini ni kutokana na idadi kubwa ya vifo nchini humo.
Takwimu zaonesha kwamba hadi kufikia Aprili 14, watu karibia 4 600 walikua wameaga dunia. Lakini kundi la watafiti wa Iran nchini Marekani linaamini kwamba kuna uwezekano mkubwa idadi kamili ya waliokufa ikawa juu zaidi.
Miongoni mwa watafiti hao ni Hazhir Rahmandad, profesa mshiriki wa Taasisi ya Kiteknolojia ya Massachusetts na Navid Ghaffarzadegan, profesa mshiriki wa chou cha ufundi cha Virginia Tech. Badala ya kutegemea tu takwimu za serikali wawili hao walitengeneza mfumo ambao unaonesha vile ugonjwa wa virusi vya corona unavyosambaa.
Makadirio yao ni pamoja na takwimu ya raia wasafiri wa Iran waliothibitishwa kuambukizwa wakati wanaingia mataifa mengine pamoja na jamii zingine kuanzia wahudumu wa afya wakati wanakusaya data zao ili kukaribia kupata twakwimu sahihi.
Kulingana na hesabu yao, hadi Machi 20, zaidi ya watu 15,000 wameuawa na idadi ya waliopata maambukizi huenda ikakaribia milioni.
-BBC
No comments:
Post a Comment