SHUGHULI KWA BAADHI YA MAJIMBO KUANZA KUREJEA MAREKANI...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 16 April 2020

SHUGHULI KWA BAADHI YA MAJIMBO KUANZA KUREJEA MAREKANI...!

Donald Trump

RAIS Donald Trump wa Marekani amesema kuwa Marekani "imefikia kilele" cha visa vya ugonjwa mpya wa Covid-19 na kutabiri kuwa baadhi ya majimbo yataondoa marufuku ya kutotoka nje na kurejea katika hali ya kawaida mwezi huu.
Katika maelezo take ya kila siku White House kuhusu ugonjwa huo, Bw. Trump amesema muongozo mpya wa kurejelea shughuli za kawaida utatangazwa siku ya Alhamisi baada ya kuzungumza na magavana.

"Tutarejelea hali ya kawaida wanangu, tena sisi sote," rais alisema. "Twataka nchi yetu tena." Marekani in a zaikai ya watu 638,000 waliothibitishwa kuwa ugonjwa wa Covid-19 na zaidi ya vifo 30,800.

"Takwimu za kitaifa zinaashiria, tumepita kilele cha maambukizi mapya ya virus vya corona," Bw Trump aliwaambia waandishi wa habari Rose Garden siku ya Jumatano. "Ni matumaini yangu tutaendelea hivyo, na tutaendelea kufanya kupiga hatua zaidi.''

Alipoulizwa Marekani ina idadi kubwa ya watu 136,908, waliofariki katakana na ugonjwa huo kote duniani, Bw. Trump alilaumu baadhi ya mataifa kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu idadi ya vifo.

"Kuna mtu anaamini idadi ya vifo vya baadhi ya nchi?" alisema, na kutaja China. Pia alisema Marekani inachunguza madai kuwa virusi vya corona vilikuzwa ndani ya maabara mjini Wuhan na kwamba chanzo chake sio soko la mji huo.

Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa ubalozi wa nchi hiyo mjini Beijing unahoji usalama wa maabara mbili iliyopo Wuhan. Hatahivyo siku ya Jumanne Jenerali Mark Milley, mwenyekiti wa pamoja wa wakuu watumishi wa umma, alisema idara ya ujasusi wa Marekani inaamini huenda janga la corona 'sio jana la kawaida'.

Utawala wa Trump uliwahi kusema kuwa Mei mosi ndio tarehe ambayo taifa hilo huenda ikarejelea hali yake ya kawaida, lakini rais alisema baadhi ya majimbo huenda yakafanya hivyo kabla ya wakati huo.

"Nafikiria itakuwa wakati wa kufurahisha sana," alisema. Alipoulizwa kuhusu hatari ya taifa hilo kuondoa marufuku ya kutoka nje mapema, Bw.Trump alisema: "Kuna hatari ya vifo ikiwa wataendelea na amri hiyo." Aligusia masuala ya afya ya akili, akisema nambari za simu ya dharura "imelipuka" huku uchumi ukisitishwa.

Mamilioni ya Wamarekani wamepoteza kazi kutokana na amri iliyowekwa ya kudhibiti maambukizi ya corona kote nchini huku viwango vya ukosefu wa ajira vikivunja rekodi. Mauzo ya bidhaa yalishuka kwa asilimia 8.7 mwezi Machi, kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu mwaka 1992, kwa mujibu wa ripoti ya serikali iliyotolewa siku ya Jumatano.

Huku hayo yakijiri Magavana katika majimbo ya Connecticut, Maryland, New York na Pennsylvania wametoa amri au muongozo wa wakazi kuvalia barakoa wanapojiandaa kurejelea shughuli zao za kawaida katika jamii wiki chache zijazo.

"Tutarejelea hali yetu ya kawaida - itakuwa kawaida mpya," Gavana wa Connecticut Ned Lamont alisema. Siku ya Jumatano, Meya wa Los Angeles Eric Garcetti alisema mikusanyiko mikubwa ya watu kama vile ya michezo na matamasha huenda isiruhusiwe katika jiji hilo hadi 2021.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema China lazima "iweke wazi" suala la coronavirus, alipo mpigia mwenzake wa Beijing, Yang Jiechi, ilisema Wizara ya mambo ya ndani chi hiyo.

Bw. Pompeo amekuwa akilaumu Beijing kwa kuficha kiwango cha mlipuko wa virusi vya corona siku za awali, madai ambayo China inapinga.

-BBC

No comments:

Post a Comment