CCM YAKEMEA UTELEKEZAJI WA WATOTO, VITUO VYA KULELEA WATOTO VYAOMBA MSAADA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 4 February 2021

CCM YAKEMEA UTELEKEZAJI WA WATOTO, VITUO VYA KULELEA WATOTO VYAOMBA MSAADA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania UWT Mkoa wa Kagera Hajati Faidha Kainamula akikabidhi zawadi za vitu mbalimbali kwa uongozi wa kituo cha Kolkata kilichopo chini ya shirika la Mother of Charity kinachopatikana Rulenge wilayani Ngara feb 03,2021.

Na Allawi Kaboyo - Ngara

VITUO vya kulelea wazee na watoto Yatima na wenye mazingira magumu Nyumba ya Malaika na Kolkata vilivyopo Rulenge wilayani Ngara vinakumbwa na changamoto ya upatikanaji wa maji pamoja na huduma nyingine za muhimu.

 

Hayo yamebainishwa na viongozi wa vituo hivyo walipotembelewa na uongozi UWT Mkoa wa Kagera Feb 03, mwaka huu kwa lengo la kuwafariji na kuwapa zawadi wakati wa maadhimisho miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.

 

Sister Mariagolet Felix ni kiongozi wa kituo cha Nyumba ya Malaika ambaye ameeleza kuwa kituo chake wanao jumla ya watoto 35 ambapo waliowengi wameshafikisha umri wa kwenda shule.

 

"Katika kituo hiki tupo masister 4 na wafanyakazi wengine wanaotusaidi 8, wengi wa watoto tulionao hapa ni wale waliotelekezwa yaani wakuokotwa ambao hawajulikani kwao ni wapi, na wengine wanaletwa na kutekelezwa, mfano tunao watoto mapacha waliletwa Wana siku moja na baba Yao Hadi Sasa wanamiaka mitatu baba Yao hajawahi kuonekana na tulipofatilia tuliambiwa alihama alipokuwa anaishi." Amesema Sister Mariagolet.

 

Sister Felix amesema kuwa kazi ya kuwalea watoto hao ni ngumu kutokana na mahitaji yao hivyo amewaomba wadau kuendelea kuwasaidia na kuitaka serikali kukemea vitendo vya kuwatelekeza watoto ambavyo hupelekea watoto kukosa haki zao.

 

Katika kituo cha Kolkata kilichopo chini Missionaries of Charity kiongozi wa kituo hicho aliyejitambulisha kwa jina la Sister Innocencia kituo kinacholea watoto na wazee amesema kuwa wanalea watu wa kada mbalimbali.

 

"Katika kituo chetu tunao watu wa Aina nne tofauti, tunao watoto ambao wanaletwa hapa kwa kukosa lishe Bora, tunao watoto mayatima na waliotelekezwa, tunao mama na mtoto ambao wametelekezwa lakini pia tunao wazee ambao pia wametelekezwa." Amesema Sister Innocencia.

 

Ameongeza kuwa katika kipindi hiki kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya maji hali inayowalazimu kutumia pesa nyingi kununua maji kwa watu wanaotembeza baada ya huduma hiyo kukatika kwa kipindi Cha takribani miezi zaidi ya sita japo wamelipia huduma hiyo.

 

Sister Innocencia ameiomba serikali kuingilia Kati suala hili ili kuweza kuwanusuru watoto maana huduma hiyo ni muhimu licha ya kuwa wamekuwa wakifanya jitihada kubwa za kurejeshewa huduma hiyo bila mafanikio na kuongeza kuwa changamoto nyingine ni Nishati ya kuni.

 

Kwaupande wake Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake wa Tanzania UWT Mkoa wa Kagera Hajat Faidhat Kainamula ameushukuru uongozi wa vituo hivyo kwa moyo wa kujitolea wa kuwalea watoto hao licha ya kuwa wao hawabebi mimba.

 

Amesema kuwa kazi hiyo ni ya utume na malipo yake watayapata kwa mungu ambapo amewaomba kuendelea kuwatunza na kuwafariji watoto hao ili na wao wajione wanawazazi.

 

Kuhusu changamoto Hajat Faidha amesema kuwa wamezichukua na kwenda kuzifanyia kazi huku akiahidi kuwa UWT Mkoa wa Kagera wataleta Gari moja la kuni ili kuweza kutatua changamoto ya kuni.

 

Hamimu Mahmudu Mjumbe wa kamati ya utekelezaji na katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kagera amelaani vikali vitendo vya wazazi wasiokuwa na utu wanaowatelekeza watoto wao ambao wamewabeba matumboni mwao kwa miezi Tisa.

 

Amesema kuwa vitendo hivyo havikubaliki na wao Kama chama tawala wanaamini kuwa binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja hivyo kila mwanadamu anayohaki ya kuishi na kuitaka serikali kuwachukulia hatua wale wote wanaobainika wamefanya vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment