RAIS SAMIA AZINDUA KITABU MIAKA 60 YA HISTORIA YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS PAMOJA NA KITABU CHA SAFARI ZA PICHA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MIAKA 60, IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 24 April 2024

RAIS SAMIA AZINDUA KITABU MIAKA 60 YA HISTORIA YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS PAMOJA NA KITABU CHA SAFARI ZA PICHA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MIAKA 60, IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wageni pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua Kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa vitabu vya Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60, Mama Hasna Kawawa mjane wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Rashid Mfaume Kawawa (kulia) na Mama Fatuma Jumbe Mjane wa Rais wa Pili wa Zanzibar Hayati Aboud Jumbe Mwinyi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.

Mmoja wa Waandishi wa Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahamoud Thabit Kombo akizungumza kabla ya uzinduzi wa Kitabu hicho kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.


Picha namba 20-21. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameshika Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 mara baada ya kukizindua kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.

No comments:

Post a Comment