NHIF TANGA WATOA HUDUMA NJE YA OFISI KUKABILIANA NA CORONA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 15 April 2020

NHIF TANGA WATOA HUDUMA NJE YA OFISI KUKABILIANA NA CORONA

 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Mtaa wa Senkrani Mohon Singh aliyefika kwenye ofisi zao kupata huduma za bima ambapo kwa sasa wanatoa huduma zao nje ya ofisi ikiwa ni sehemu ya kupunguza mkusanyiko na kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa unaitikisa dunia.

 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akimsikiliza mmoja wa wateja wao leo wakati wakitoa  huduma nje ya ofisi zao ikiwa ni sehemu ya kupunguza mkusuanyiko na kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa unaitikisa dunia.

 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akimsikiliza mteja wao kama alivyokutwa.

 Huduma zikiwa zinaendelea kwenye ofisi za nje kama inayoonekana huku wateja wengine wakiwa foleni.



Afisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Mrisho Mponela akiendelea na kazi nje ya ofisi zao.

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga umelazimika kuhamishia ofisi zake nje ili kuweza kutoa huduma kwa wananchi wanaokwenda ikiwa ni sehemu ya kupunguza mkusanyiko na kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa unaitikisa dunia.

Blog ya Kijamii ililishuhudia baadhi ya huduma zikitolewa nje ya ofisi na wananchi wakiendelea kupata huduma mbalimbali ambapo Meneja wa NHIF Mkoa wa Tanga Ally Mwakababu alikuwa akiongoza zoezi la kusikiliza wateja.

Akizungumza na Blog hii Meneja wa NHIF Mkoa wa Tanga Ally Mwakababu alisema kwamba dhamira kubwa ni kuonyesha jamii juu ya kujali na kupambana na ugonjwa wa Corona lakini pia kuwasiliana na wateja wao kwenye eneo lenye nafasi kubwa kwenye hewa kuliko kufanya kazi kwenye ofisi ambapo wanakuwa wamejifungia.

Alisema hapo kila mtu anakaa kwenye nafasi yake kwa mita mbili na mita moja na nusu kati ya mtu na mtu na mazingira salama na wanapata hewa nzuri kutokana viti kuwa mbalimbali ili kuweza kuwafanya wateja kuwa kwenye mazingira mazuri ikiwemo eneo ambalo watu wananawa mikono kwa kutumia sanitize ambayo kila anakuja kuhudumiwa anapatiwa.

Alisema kwamba wao kama mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni kiio kwa na kuonyesha kuitikia mwito wa serikali kupitia Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwamba suala la ugonjwa wa Corona sio la utani tena ni lazima lichukuliwe kwa umakini mkubwa.

“Hivyo kutokana na hilo na ndio maana tumeamua kutoa ofisi nje kwa lengo la kuweza kuwasiliana na wateja wetu kwenye eneo kubwa na kila mtu anakaa kwa nafasi kwa mita mbili au moja na nusu lakini mazingira salama huku kila mtu anayekwenda kuhudumiwa lazima anaweze kunawa mikono kwa kutumia Santinze”Alisema Meneja Mwakababu.

Hata hivyo alisema kwamba pamoja na kuendelea kutoa huduma mbalimbali lakini eneo kubwa ambalo wanalihimiza ni mpango wa toto afya kadi ambao unawawezesha watoto kuweza kunufaika na matibabu pindi wanapokuwa wakiugua hivyo wameendelea kulihamasisha kwenye maeneo mbalimbali.

Meneja huyo alisema kwamba dhamira kubwa ya mfuko huo ni kuhakikisha inawafikia wananchi wote kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga ili waweze kujiunga nao na hatimaye kuweza kunufaika na huduma za matibabu pindi wanapokuwa wakiugua.

No comments:

Post a Comment