Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Iringa Constatine Kihwele akikabidhi msaada huo kwa wananchi wa kitongoji cha Mbingama waliokumbwa na mafuriko kutokana na mvua nyingi za msimu huu.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
CHAMA cha mapinduzi wilaya ya
Iringa imetoa msaada wa chakula,Nguo na sabuni kwa wahanga wa kuziwezesha kaya
zilizokumbwa na mafuriko katika kitongoji cha Mbingama kijijini Isele, tarafa
ya Pawaga wilayani Iringa kukabiliana na changamoto ya ambazo nwanakabilia.
Msaada huo unaohusisha unga na
maharage ulikabidhiwa kwa mwenyekiti wa kijiji cha Isele kwa niaba ya wahanga
hao wa mafuriko katika kitongoji cha Mbingama.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
msaada huu mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Iringa Constatine Kihwele
alisema mafuriko yaliyotokea hivikaribuni katika kitongoji hicho yamesebabisha
kaya 218 zenye jumla ya watu 801 kuachwa bila makazi huku akiba yao ya vyakula,
fedha, nguo na vifaa vyao vingine vikisombwa baada ya nyumba zao kubomoka.
Kihwele alisema kuwa chama cha
mapinduzi,serikali na wadau wengine wataendelea kutafuta msaada wa kuwasaidia
kutokana na kukumbwa na mafuriko ambayo hawakutarajia.
Aliwataka wadau mbalimbali
kuendelea kutoa msaada kwa wahanga hao wa mafuriko kwa kuwa bado wanamahitaji
mengi ambayo wanatakiwa kusaidiwa kutokana na kupoteza asilimia kubwa ya mali
zao ambazo walikuwa wanamiliki kabla ya kukumbwa na mafuriko hayo.
Kihwele aliwataka wananchi wa
kitongoji hicho kilichokumbwa na mafuriko kuendelea kujikinga na ugonjwa wa
Corona licha ya kuwa bado wapo katika kipindi kigumu kutokana na mafuriko
yaliyowapata.
Naye mwenyekiti wa umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa Makalah Mapesa aliwataka wahanga
hao wa mafuriko kuanza kutafuta njia ya kujitegemea kwa kuwa msaada huu itafika
mahala utaisha na hakutakuwa na mtu wa kusaidia tena.
“Naomba muanze kujifunza
kujitegemea kwa kuwa hii misaada tunayoileta hizi saizi inamwisho wake ni bora
kuanza kutafuta njia mbadala ya kuanza kuishi maisha yenu ya kawaida kama
ambavyo mlikuwa mnaishi hapo awali” alisisitiza Mapesa
Mapesa alisema kuwa hakuna watu
ambao watapewa msaada wa maisha kutokana na kukumbwa na mafuriko hivyo ni bora
mkautumia vizuri msaada ambao mnapewa na wadau mbalimbali.
Katika msafara wa kwenda kutoa
msaada huo waliambatana na madiwani wanawake wa chama cha mapinduzi wilaya ya
Iringa pamoja na katibu wa mbunge wa jimbo hilo Thom Lukuvi
No comments:
Post a Comment