Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Ryata akiwa anatekeleza tukio la kupulizia dawa ya kutokomeza virusi vya Corona kwa lengo la kuwapa uhuru wafanyabiashara wadogo kufanya biashara kwa lengo la kukabiriana na maambukizi.
Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Ryata akipulizia dawa kutokomeza virusi vya Corona katika eneo la stand ya Daladala Manispaa ya Iringa.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
WAFANYABIASHARA wadogo wadogo wa
soko la Mashine Tatu maarufu kama Machinga mkoani Iringa wameiomba Serikali
kupitia wataalam wa Afya kuongeza kasi ya uelimishaji wa namna sahihi ya
kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona ili kuwaepusha wafanyabiashara hao
na wateja wao kupatwa na maambukizi.
Wakizungumza na blog hii miongoni
mwao wameeleza kuwa kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo katika eneo hilo
baadhi ya wateja na hata wafanyabiashara wamekuwa wakipuuza baadhi ya maelekezo
ya kujikinga na maambukizi hali inayozua hofu endapo akitokea mgonjwa mwenye
Virusi vya Corona.
Aidha kwa upande wa katibu mkuu wa
Mtandao wa Machinga mkoani Iringa Joseph Kilienyi Mwanakijiji ameipongeza
Serikali ya mkoa kwa hatua za awali huku akitoa mwito kwa wadau kuangalia namna
ya kusaidia upatikanaji wa vifaa ikiwemo ndoo na sabuni ili viongezwe ili
kukidhi mahitaji halisi.
Kirienyi amesema kuwa licha ya
Serikali kutoa elimu na kuwapatia baadhi ya vifaa bado uhitaji ni mkubwa hasa
katika eneo hilo la soko la mashine tatu kutokana na idadi ya watu wanaoingia
na kutoka kwa ajili ya mahitaji mbalimbali kupindukia Elfu sita kwa siku.
Hata hivyo amesema wameendelea
kushirikiana na Serikali kwa kuwahimiza wafanyabiashara kuzingatia taratibu
zote za msingi ikiwemo ya kuwakumbusha wateja wao kuosha mikono na kuepuga
kugusana pamoja na tahadhali nyingine kama Serikali Ilivyoagiza.
Aidha kwa upande wake Meya wa
Manispaa ya Iringa Joseph Nzala Ryata akizungumzia hatua walizochukua mpka hivi
sasa ni pamoja na kuwatumia watu wenye ushawishi zaidi kwenye jamii ikiwemo
viongozi wa kidini na wazee wa kimila kwa ajili ya kuelimisha umma kupitia
nafasi zao.
Kuhusu maeneo ya kibiashara Ryata
amekiri kuwapo kwa changamoto ya elimu na muitikio sahihi hasa maeneo kama ya
masoko likiwemo hilo la mashine tatu lakini ameeleza kuwa Manispaa imebandika
matangazo yanayoonesha hatua muhimu za kuzingatia kijikinga na Virusi hivyo
hatari vinavyosababisha maradhi ya Covid 19.
Aidha Meya Ryata amesisitiza
kuwa kwa sasa wameendelea kuwasiliana na Viongozi wa makundi mbalimbali kwa
ajili ya kusikia changamoto zilizopo hasa katika kipindi hiki kusikia maoni yao
na kuwashari mambo ya kufanya ili kila mmoja awe wa kwanza kujilinda na
maambukizi ya corona hatua itakayowaidia kuendelea kufanyabiashara zao huku
wakijilinda na hatari ya maambukizi.
No comments:
Post a Comment