WAZEE WA KIMILA SINGIDA WAOMBWA KULIOMBEA TAIFA JUU YA UGONJWA WA CORONA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 17 March 2020

WAZEE WA KIMILA SINGIDA WAOMBWA KULIOMBEA TAIFA JUU YA UGONJWA WA CORONA

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Meya wa Manispaa ya Singida,  Alhaji Mbua Chima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtamaa.

 Wazee wa kimila wakiwa kwenye mkutano wa Meya.

Wazee wa kimila wakimkabidhi Meya zana za kimila.
Na Mwadishi wetu, Singida
WANANCHI wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona ambao unaonekana kuwa tishio na janga la kidunia.
Meya wa Manispaa ya Singida,  Alhaji Mbua Chima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtamaa ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya ilani ya uchanguzi kwenye kata hiyo ya miaka mitano ya utekelezaji wakati alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara. 
“Nawashukuru sana wananchi  kwa kuniunga mkono katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezi wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 
Kwa pamoja tumeweza kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo hasa katika kata yetu hii-tumeweza kutatua changaomoto mbalilmbali kama maji, elimu, barabara, afya na kuwapatia mikopo vikundi vya kinamama na vijana zaidi ya milioni kumi na saba zimetolewa Halmashauri ya Manispaa ya Singida.” alisema
Aidha Meya ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuipatia kituo cha afya kata hiyo ambacho  kinatoa huduma bora kwa wananchi na kuondoa malalamiko yaliyokuwepo awali.
“Nimejaribu kuunga mkono shughuli mbalimbali za kijamii kama diwani wenu, nimetoa mipira kwenye shule zetu zote, nimechangia zaidi ya milioni moja kwenye maendeleo ya kata yetu katika nyaja mbalimbali.”alisema Meya 
Hata hivyo Meya huyo amewakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pamoja na wale wenye imani  kuendelea kumuomba mwenyezi Mungu na  wazee wa kimila kuingilia kati ili kuzuia janga la ugonjwa wa corona. 
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa kata hiyo,  Boniphace Ipini amesema kwa kushirikiana na watendaji wa vjiji wanaendelea kuchukua tahadhari hasa kwenye minada ambapo kunakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Tunatengenza mabango ya kutoa ujumbe wa tahadhari ya ugonjwa huu na tutatenga sehemu za kunawia mkono katika maeno yote ya mikusanyiko ya watu  na maofisini.
Kwa upande wao wananchi wamemshukuru sana diwani huyo ambapo wamesema amejitahidi kutimiza ahadi zake japo hajazimaliza zote.
“Tunamshukuru  Rais wetu Dkt. John  Magufuli kwa kutuletea kituo cha afya na wataalamu kwasasa tunapa huduma bora na kwa wakati  tofauti na mwanzoni.” walisema wananchi.

No comments:

Post a Comment