WANASIMBA NA WANAHABARI NCHINI WAPATA PIGO...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 26 March 2020

WANASIMBA NA WANAHABARI NCHINI WAPATA PIGO...!

ASHA MUHAJI 

MASHABIKI wa Timu ya Simba, SSC pamoja na waandishi wa habari za michezo nchini wamepata pigo kubwa baada ya mwanadada ASHA MUHAJI kufariki dunia katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.


Marehemu Asha ambaye kitaaluma ni mwanahabari aliyebobea katika uandishi habari za michezo na aliyewahi kuwa Msemaji wa club ya Simba hapo nyuma amekumbwa na umauti katika hospitali hiyo leo alipokuwa akipatiwa matibabu.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki wa Simba Sports Club amesema kifo cha Asha kimetokea majira ya mchana na msiba upo Kijitonyama karibu na Kanisa la KKKT mkabala na Kituo cha Police Mabatini.


"Mwili wa dada yetu utasomewa Dua kesho mchana nyumbani kwake kuanzia saa 7 mchana baada ya hapo utapelekwa Msikiti wa Mwinyi Mkuu Magomeni Kusaliwa na mwisho utahifadhiwa Magomeni katika makaburi ya Mwinyi Mkuu," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Simba, Haji Manara imewataka wanasimba popote walipo kushiriki kikamilifu kumsindikiza mwanasimba huyo kindakindaki ili kuonesha umoja wao na mchango wake kwenye club hiyo kabla ya umauti kumkumba.

No comments:

Post a Comment