TIMUZA DHARURA ZA KUKABILI MAGONJWA AMBUKIZI YA MLIPUKO ZATAKIWA KUTUMIA DHANA YAAFYA MOJA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 17 March 2020

TIMUZA DHARURA ZA KUKABILI MAGONJWA AMBUKIZI YA MLIPUKO ZATAKIWA KUTUMIA DHANA YAAFYA MOJA

Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akisisitiza umuhimu wa kutumia Dhana ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu wakati wa mafunzo kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko leo, Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.

Mratibu wa Mradi wa ECTAD Tanzania kutoka FAO, Fasina Folorunso akisisitiza umuhimu wa kuimarisha Afya ya Binadamu kwa sekta za Afya kutumia Dhana ya Afya Moja, wakati wa mafunzo kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ya ambukizi ya mlipuko leo, Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.

Mkuu wa Ndaki ya Mifugo, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine-SUA, Profesa, Amandus Muhairwa akisisitiza sekta ya Afya ya mifungo na Afya ya Binadamu, kushirikiana katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu wakati wa mafunzo kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko kwa kutumia Dhana ya Afya moja  leo, Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.

Mkufunzi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Selemani Makungu, akieleza jambo wakati wa mafunzo kwa  wataalamu wa sekta za Afya kutoka kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ya mlipuko kutoka ngazi ya mkoa na wilaya zilizo mipakani, kwa kutumia Dhana ya Afya moja, wakati wa mafunzo hayo, leo Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.


Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya kutoka kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ya mlipuko kutoka ngazi ya mkoa na wilaya zilizo mipakani, wakifuatilia mafunzo ya kukabili magonjwa ya ambukizi ya mlipuko kwa kutumia Dhana ya Afya moja, wakati wa mafunzo hayo, leo Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.

DHANA ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu imeendelea kufundishwa kwa Wataalamu wa sekta hizo za Afya, ikiwa ni Sekta ya Afya  ya Binadamu, Wanyamapori, Mifugo, Kilimo na Mazingira, ili wataalamu hao watumie dhana hiyo kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama  ambayo hutokea mara kwa mara katika maeneo ya mipakani kutokana na kuwepo kwa  muingiliano mkubwa kati ya  watu na wanyama katika mazingira yao.

Katika kuimarisha Afya ya binadamu, Shirika la Chakula na Kilimo  la Umoja wa Mataifa (FAO), pamoja  na watalaamu kutoka Wizara ya Mifugo na  Uvuvi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wamewapa mafunzo wataalamu wa sekta za Afya wanao toka katika Halmashauri za Mkoa wa Kagera, Rukwa, Katavi,  Rukwa na Songwe zilizo mipakani juu ya namna ya kujiandaa na kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko kama  vile Ugonjwa wa Corona na Ebola kwa kutumia Dhana ya Afya  moja.

Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo leo tarehe 17 Februari, 2020, Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa  Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, amebainisha kuwa ushirikiano wa wataalam na sekta za Afya  kwa kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya dunia nzima. Aidha, ameeleza kuwa Dhana hiyo imekusudiwa kutumika maeneo ya mipakani   ambapo mwingiliano huo huchochewa na wasafiri kutoka eneo moja kwenda jingine, ongezeko la watu duniani, mabadiliko ya tabia nchi, utandawazi, ongezeko la mahitaji ya maji na chakula.

“Mafunzo haya  ni  muhimu sana nchini kwa kujenga uwezo wa nchi katika utayari wa kukabiliana na magonjwa yanayosambazwa na wanyama na kuathiri wanyama na binadamu.Tanzania tumeabiwa yupo mgonjwa wa Corona19, ambapo Tumeambiwa mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu, na serikali inaendelea kuchukua hatua za madhubuti za kuhakikisha ugonjwa huu unadhibitiwa ili usisambae nchini”.

Awali akiongea katika mafunzo hayo, Mkuu wa Ndaki ya Mifugo, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine-SUA, Profesa, Amandus Muhairwa amebainisha kuwa  sekta za Afya zikishirikiana katika Kudhibiti magojwa zitasaidia kuimarisha Afya ya Binadamu kwa kuwa kila sekta itakuwa inachukuwa tahadhari kwa wakati.

Aidha, Mratibu kutoka FAO wa Mradi wa  ECTAD Tanzania, Fasina Folorunso amabainisha kuwa FAO inaendelea kushirikiana na serikali mya Tanzania kupitia Dawati la  Afya moja katika kujenga uwezo wa kukabiliana na magonjwa ambukizi ya mlipuko kwenye ngazi ya mkoa na wilaya hususani maeneo ya mipakani.

Katika kuhakikisha watalaam hao kutoka sekta za Afya wanaweza kutumia Dhana  hiyo katika kudhibiti magonjwa katika maeneo ya mipakani wameweza kujengewa uwezo wa namna ya kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa ambukizi kama vile ugonjwa wa Corona 19 na Ebola  yanapotokea maeneo ya mipakani, namna ya kuunda vikosi vya kufuatilia na kukabili Ugonjwa, Mawasiliano wakati wa kufuatilia na kukabili magonjwa hayo kwa kutumia Dhana ya Afya moja,  pamoja na masuala ya kutumia vifaa Kinga Binafsi vya Kitaalamu.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wakishirikiana na USAID, OIE, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine - SUA wakishirikiana na Chuo Kikuu cha Kansas cha nchini Marekani waliandaa na kuratibu mafuzo hayo.

No comments:

Post a Comment