Mkuu wa wilaya ya iringa Richard Kasesela akitoa maagizo kwa wadau wa sekta ya afya juu ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Corona.
Mkurugenzi wa kiwanda cha uzalishaji wa maziwa kampuni ya Asas mkoani Iringa Ahmed Asas na wadau wengine wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa maagizo juu ya virusi vya Corona.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
SERIKALI ya wilaya ya
Iringa imepiga marufuku sherehe zote harusi ambazo hazina kibali maalumu kutoka
kwa Mganga mkuu wa wilaya (DMO) kutokana na kuwepo kwa tishio la maambukizi ya
virusi vya Corona nchini.
Akizungumza
kwenye kikao cha wadau wa sekta ya afya,mkuu wa wilaya ya iringa Richard
kasesela alisema kuwa sherehe zote za harusi haziruhusiwi kufanyika bila kupata
kibari maalumu kwa lengo la kulinda afya za wananchi wanaokuwa wanasherekea
harusi kutokana na kuwepo kwa tishio la maambukizi ya virusi vya corona.
Ni lazima
kila sherehe katika wilaya ya Iringa kuwepo mfumo wa kusafishia mikono kwa
lengo la kukwepa maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimekuwa tishio
hapa nchini na duniani kwa ujumla.
Kasesela
alisema kuwa kwenye harusi huwa kuna kuwa na mkusanyiko wa watu wengi hivyo ni
lazima kuweka king a mapema ili yasitokee maambukizi makubwa kama ambayo
yametokea nchi nyingine.
Aisha
kasesela aliwataka wananchi wa wilaya ya Iringa kuwa makini na mikusanyiko ya
watu ili kuepuka kupata maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimekuwa
vinatishia uhai wa wananchi.
"Misiba,kusalimia,vituo
vya usafiri,makanisani na misikitini ni lazima kuondokana na Mira na tamaduni
zetu ambazo tumekuwa tumezizoea ili kuepukana na maambukizi ya virusi vya
corona" alisema kasesela
Kasesela
alitaka halmashauri zote za wilaya ya Iringa kuhakikisha kwenye vituo vya
afya,vituo vya mabasi,maduka makubwa,kampuni mbalimbali zote lazima kuwe na
sehemu za kunawia mikono ili kuepuka na maambukizi ya virusi vya corona.
"Iringa
hakuna hata mgonjwa mmoja wa maambukizi ya virusi vya corona na taarifa
zinazoenea sio za kweli wananchi wa iringa wanatakiwa kuzipuuza na mwenye
jukumu la kutangaza uwepo virusi hivyo ni waziri husika au viongozi wa ngazi za
juu"alisema kasesela
Kwa upande
wake mdau wa sekta ya afya mkoani Iringa Ahmed Asas alisema kuwa wamekuwa
wakitoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya corona kwa waandishi wa
habari,wafanyakazi wa kampuni ya Asas na taasisi binafsi kwa lengo la kuepuka
kuambukizwa virusi vya corona.
Ahmed alisema
kuwa kwenye kampuni ya Asas wamefanikiwa na kuwa na chumba maalumu kwa ajiri ya
wafanyakazi watao kuwa na dalili za maambukizi ya virusi vya corona na
wameganikiwa kutoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi kwa lengo la kuwa msaada kwa
wafanyakazi wengine.
"Sisi
tupo tayari kutoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya corona sehemu yeyeyo
ile kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ya Iringa kama ambavyo yumeanza na
mkuu wa mkoa wa Iringa Richard kasesela" alisema Ahmed
Naye mganga
mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Samwel Marwa alisema kuwa wamejipanga kila idara
kuhakisha wanatoa elimu na kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
No comments:
Post a Comment