Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa TCRA, Francis Mihayo akizungumza katika semina ya Kamati ya Amani Mkoa Kagera kuhusiana na Kampeni ya TCRA ya Sirubuniki Mjanja haingizwi Chaka. |
Sheikh wa Mkoa wa Kagera na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa huo, Haruna Kichwabuta akizungumza katika semina ya viongozi wa dini kuhusiana na Kampeni ya TCRA Sirubuniki Mjanja haingizwi Chaka. |
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Joshua Mwangasa akizungumza kuhusiana na makosa ya mitandao viongozi wa dini Mkoa wa Kagera katika Kampeni ya Sirubuniki Mjanja haingizwi Chaka. |
Baadhi wa dini wa Kamati ya Amani Mkoa wa Kagera. |
Baadhi wa dini wa Kamati ya Amani Mkoa wa Kagera. |
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya amani Mkoa wa Kagera. |
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora ameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuja na kampeni ya sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka.
Profesa Kamuzora ameyasema hayo wakati akifungua semina ya Kamati ya Amani Mkoa wa Kagera iliyoandaliwa na TCRA kutoa Elimu ya Kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.
Katibu Tawala hiyo amewaomba viongozi wa dini kuiunga mkono Serikali kupitia TCRA kueneza elimu ya mawasiliano. Amesema viongozi wa dini wana wanaumini wengi hivyo ni rahisi kufikisha elimu hiyo kwa haraka.
"Ninaamini viongozi wa Dini mkivalia njuga basi watu wataweza kujikinga na uhalifu wakati wa wanaotumia huduma za mawasiliano." Amesema Profesa Kamuzora.
Naye Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo amesema viongozi wa dini ni kiungo muhimu katika kuwa daraja la kufikisha taarifa kwa haraka na wanaaminiwa zaidi na watu.
Mihayo amesema semina ya viongozi wa dini itazaa matunda kwa wananchi kuwa na uelewa namna ya kutumia mawasiliano. Aidha amesema kuwa Kanda ya Ziwa itaendelea kutoa Elimu ya Mawasiliano katika Kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.
Kampeni ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania. Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo la kujenga maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali
Naye Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA, Mabel Masasi amebainisha kuwa lengo la TCRA ni kufikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka, na kuongeza kuw wakati umefika wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi pamoja na wanaotumia bila kufuata sheria na taratibu mkono wa sheria kuchukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment