Mkuu wa mkoa wa
Iringa Ally Hapi akikagua miundombinu ya soko kuu la Mafinga wilaya ya Mufindi wakati wa ziara ya Iringa mpya awamu ya pili.
Mkuu wa mkoa wa
Iringa Ally Hapi akikagua miundombinu ya soko kuu la Mafinga wilaya ya Mufindi wakati wa ziara ya Iringa mpya awamu ya pili akiwa na viongozi wa mkoa wa Iringa na wilaya ya Mufindi.
NA FREDY MGUNDA,MAFINGA.
WAFANYABIASHA wa soko kuu la Mafinga
mkoani Iringa wamelalamikia kukosekana kwa huduma bora ya choo kwa kuwa
inahatarisha afya za wafanyabiashara hao.
Hayo yameibuka wakati wa ziara
ya mkuu wa mkoa wa Iringa alipotembelea soko hilo kwa lengo la kukagua
miundombinu na maendeleo ya wafanyabiasha wa soko hilo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa
soko hilo walisema kuwa wamekuwa wanachangia kiasi cha shilingi mia kila anapokwenda
kupata huduma hiyo,lakini choo hiyo inahari mbaya ya kimiundombinu kiasi cha
kusababisha magonjwa kwa watumiaji wa huduma hiyo ya choo.
Akijibia hoja mkuu wa mkoa wa
Iringa Ally Hapi aliutaka uongozi wa soko kuu la Mafinga kutumia siku tatu
kuhakikisha wanatatua tatizo la huduma ya choo ambayo imekuwa kero kwa
wafanyabiashara wa soko hilo.
Alisema kuwa wafanyabiashara
wanalipia fedha kupata huduma hiyo ya choo lakini mazingira sio salama kulinga
na thamani ya ambayo inatolewa na watumiaji wa huduma hiyo.
“Haiwezekaji kila mwezi
mnapokea zaidi ya shilingi laki tisa lakini mnashindwa kuboresha huduma kwa
wanyabiashara wa soko hivyo natoa siku tatu tu kuhakikisha wanaboresha huduma
hiyo la sivyo ataufuta uongozi huo” alisema Hapi
Hapi alisema kuwa uongozi
unatakiwa kujenga choo kipya na bora ili kuboresha huduma ya choo,kwa kuwa kila
mfanyabiasha hulipa kiasi cha shilingi mia moja
na tayari wameshalipa kiasi cha shilingi elfu kumi na zinatosha kabisa
kuboresha huduma hiyo.
Aidha Hapi alimtaka mkurugenzi
na uongozi wa soko kuhakikisha wanatatua tatizo la takataka,choo na vibanda vya
kufanyia biashara kwa kuwa vimekuwa kero kwa wafanyabiasha wa soko hilo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
halmashauri ya Mji wa Mafinga Sada Mwaruka alisema kuwa watahakikisha wanatatua
kero hizo kwa lengo la kuhakikisha wanaboresha huduma ya soko kuu hilo la
mafinga.
No comments:
Post a Comment