KUSAYA, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO - ILI TAASISI ZA KILIMO ZIENDELEE KUWEPO NI LAZIMA ZITEKELEZE MAJUKUMU YAKE IPASAVYO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 11 March 2020

KUSAYA, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO - ILI TAASISI ZA KILIMO ZIENDELEE KUWEPO NI LAZIMA ZITEKELEZE MAJUKUMU YAKE IPASAVYO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akisisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma Leo Tarehe 11 Machi 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt Geoffrey Mkamilo (Kushoto) akitoa maelezo ya awali kuhusu Taasisi hiyo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya (Katikati) wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma Leo Tarehe 11 Machi 2020. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti Wizara ya Kilimo DktWilhelm Mafuru (Kulia).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akisisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma Leo Tarehe 11 Machi 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt Geoffrey Mkamilo wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma Leo Tarehe 11 Machi 2020.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akizungungumza na Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma Leo Tarehe 11 Machi 2020.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Taasisi zilizopo Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi za Mazao zimetakiwa kufanya kazi kwa Bidii na utashi mkubwa ili kutekeleza matakwa na taswira ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya ameyasema hayo Leo Tarehe 11 Machi 2020 wakati akizungumza na Uongozi na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo eneo la Makutupora Jijini Dodoma.

Kusaya amesisitiza kuwa wataalamu hao wanapaswa kufanya Utafiti na kuonyesha matokeo chanya ya utafiti huo, Ameongeza kuwa utafiti haupaswi kuishia kwenye makaratasi pekee bali matokeo chanya kwa wakulima.

Amesema kuwa Wizara ya Kilimo inashika nafasi ya pili kwa kuwa na wasomi wengi kwa ngazi za PHD na Maprofesa hivyo taaluma hiyo inapaswa kuwa na matokeo chanya kwani kutokuwa na matokeo hayo ni kazi bure kwa wananchi na uwepo wa taasisi hiyo.

Kuhusu Changamoto ya fedha kwa ajili ya utafiti wa Mazao iliyobainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt Geoffrey Mkamilo, Katibu Mkuu huyo amesema kuwa hakuna mafanikio ya kilimo bila kuimarisha utafiti hivyo lazima kutafuta njia ya kupata fedha kwa haraka ili kuendeleza utafiti.

Kusaya ametoa mwito kwa wafanyakazi wa TARI kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiendeleza kielimu. "Taasisi ya utafiti ni muhimu sana kwa watu kujielimisha zaidi, Hata kama una miaka 60 sisi tutakupeleka shule, hakuna kada ambayo tutaiacha zote tutazipeleka shule ili tuweze kwenda na wakati" Alikaririwa Katibu Mkuu Ndg Kusaya

Hii ni ziara ya kwanza ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya tangu alipokabidhiwa kijiti kuiongoza wizara hiyo kama mtendaji Mkuu Machi 6, 2020.


No comments:

Post a Comment