KAMPUNI YA PLANET YATOA MSAADA WA VITAKASA MIKONO KWA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA COVID 19 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 25 March 2020

KAMPUNI YA PLANET YATOA MSAADA WA VITAKASA MIKONO KWA SERIKALI KATIKA KUPAMBANA NA COVID 19

Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akiongea na wadau waliofika kutoa msaada wa vifaa vya kukabiliana na Ugonjwa wa Covid 19 ikiwemo Dawa ya kuulia bacteria Maalum ya kunawa mikono kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha. 

Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akipokea vifaa vya hivyo vya kutakasa mikono  kutoka kwa Meneja wa kampuni ya Planet phamasetcal limited, Joseph Lekumok ikiwa ni katika kusaidiana na Serikali kutatua Janga la Ugonjwa wa Covid 19 kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha 

WADAU wa maendeleo mkoani Arusha, wametoa misaada ya vitakasa mikono vyenye thamani ya shilingi  milioni 3.9 kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.

Akikabidhi msaada huo kwa uongozi wa Mkoa wa Arusha, Meneja wa Kampuni ya Planet Pharmaceutical limited, Joseph Lekumok, amesema msaada hio ni sehemu ya mchango kusaidia kukabiliana na ugonjwa wa Corona ambsolo ni janga la ulimwengu.

Akipokea msaada huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega amesema mkoa bado unauhitaji wa misaada mbalimbali ikiwemo vitakasa mikono kwa ajili ya kukinga wananchi dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Amewapongeza baadhi ya wadau wakiwemo Benki ya CRDB na hifadhi za taifa, Tanapa, kwa misaada yao katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona,na akatumia fursa hiyo kuwaomba wadau wengine kutoa misaada yao.

Kuhusu mkoa kutekeleza maelekezo ya kutenga maeneo maalumu ya wagonjwa wa Corona, kutoka kwenye nchi zenye ugonjwa huo, amesema tayari mkoa umeshatenga maeneo ya kutosha kwa ajili ya wote watakaogundulika kuwa na maambukizi ya Corona.

Amesema wote watakaokutwa na maambukizi watawekwa kwenye maeneo hayo yaliyotengwa ambayo watakaa humo kwa muda wa siku 14, kwa gharama zao wakati wakipata matibabu mpaka wataalamu wa afya watakapoona afya zao zimetengemaa lengo ni kuzuia maambukizi kwa wengine.

Amesema hadi kufikia Marchi 24 mkoa ulikuwa haujapokea mgonjwa wa Corona na Serikali inaendelea kufuatilia taarifa kwenye maeneo yote ya mipakani na viwanja vya ndege ili kuwatambua na kuwadhibiti, wote wanaoingia nchini  kama wana maambukizi ya Corona.

No comments:

Post a Comment